1,1-DIMETHYLHYDRAZINE ICSC: 0147
Aprili 1994

Dimethylhydrazine
N,N-Dimethylhydrazine
CAS # 57-14-7 C2H8N2 / NH2-N(CH3)2
RTECS # MV2450000 Masi ya molekuli: 60.1
UN # 1163
EC # 007-012-00-5
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua sana. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara. Usigusishe na vioksidishaji.
Poda, povu linalokinza alkoholi, maji mengi, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka. Hatari ya moto na mlipuko.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. USITUMIE hewa iliyoshindiliwa kujaza, kutoa au kuchukua.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Msokoto wa tumbo. Mchomo. Kikohozi. Kuumwa kichwa. Kupumua kwa shida. Kichefuchefu. Kuumwa koo. Kutapika.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Mibabuko ya ngozi. Maumivu. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Kwanza suuza kwa maji mengi, halafu vua nguo zilizosibikwa na suuza tena. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Maumivu. Kiwaa. Upofu wa kudumu. Kuungua kunakopenya sana.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Degedege. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vya iso-plastiki vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usifyonze katika vumbi la mbao au vifyonzi vinginevyo viwakavyo. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa.
Ainisho ya EU
Alama: F, T, N
R: 45-11-23/25-34-51/53
S: 53-45-61
Angalia: [E]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Jasara tanzu za UN: 3 na 8
Kikundi Ufungashaji cha UN: I
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GTFC-I
Msimbo wa NFPA : H 3; F 3; R 1;
Isodhurika kwa moto. Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, asidi kali. Weka gizani. Usihifadhi kwenye vyombo vya shaba au aloi zenye shaba nyingi au vyombo vya plastiki.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
1,1-DIMETHYLHYDRAZINE ICSC: 0147
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KIRISHAI, ISO RANGI NA KIFUKACHO , CHENYE HARUFU KALI. HUGEUKA MANJANO INAPOFIDULIWA NA HEWA.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii huweza kuwaka papo hapo inapogusana na hewa. Inapowaka hutengeneza mafusho yenye sumu na yanayoweza kuwaka kama vile oksidi za nitrojeni, hidrojeni, amonia, dimithiliamini na asidi hydrazoic. Dutu hii ni kinakisishaji kikali na humenyuka kwa ukali sana ikiwa na vioksidishaji kama vile tetroksidi nitrojeni, peroksidi hidrojeni na asidi nitriki. Dutu hii ni besi kali humenyuka vikali ikiwa na asidi na husababisha ulikaji. Humenyuka pamoja na oksijeni kusababisha athari ya moto na mlipuko. Hushambulia plastiki.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 0.01 ppm kama TWA; (ngozi): A3; (ACGIH 2004).
MAK: kuingia kupitia kwa ngozi (H); kuhisisha ngozi (Sh); Aina ya sarakani: 2; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi ya mvuke wake kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva na ini, kusababisha kutoweza kupumua na kuharibika kwa ini. Mfiduo wa mvuke huweza kusababisha kifo.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa neva, ini na damu. Dutu hii ina uwezekano wa kusababisha kansa kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 63°C
Kiwango myeyuko: -58°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.8
Umumunyifu katika maji: vizuri sana
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 16.4
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.1
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.2
Kiwango cha kumweka: -15°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 249°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 2-95
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -1.9
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa samaki.
VIDOKEZO
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika.Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu.Matumizi ajilani ya mnyunyuzio mwafaka unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika.Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi.Suuza nguo zilizosibikwa (hatari ya moto) kwa maji mengi.Aerozine-50 na Dimazine ni majina ya kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005