2,4-DICHLOROANILINE ICSC: 0141
Oktoba 2000

Aniline, 2,4-dichloro-
1-Amino-2,4-dichlorobenzene
2,4-Dichlorobenzenamine
CAS # 554-00-7 C6H5Cl2N
RTECS # BX2600000 Masi ya molekuli: 162.02
UN # 1590
EC # 612-010-00-8
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni. Ukanzaji unaweza kusababisha ongezeko la kanieneo na kuleta athari ya kupasuka.
Usiwashe moto.
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizo wa maji, dioksidi kaboni.
MLIPUKO

Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!

Kuvuta pumzi Ngozi kugeuka kuwa bluu. Midomo au kucha kugeuka kuwa bluu. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kukosa pumzi. Kuchanganyikiwa. Degedege. Kupoteza fahamu.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. (Tazama Kuvuta pumzi).
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, au kingao cha uso.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoa vyanzo vyote vya moto. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: T, N
R: 23/24/25-33-50/53
S: (1/2-)-28-36/37-45-60-61
Angalia: [C]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC (R)-61GT2-II
Msimbo wa NFPA : H 3; F 1; R 0;
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, vyakula na malisho.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
2,4-DICHLOROANILINE ICSC: 0141
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE ISO RANGI, YENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana ifikapo 370°C inapokanzwa au inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu pamoja na oksidi za nitrojeni, kloridi hidrojeni - tazama ICSC0163.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki
MAK haifahamiki
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kupitia katika ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera kidogo ngozi. Dutu hii huweza kuathiri damu, kusababisha kufanyika kwa methemoglobini. Mfiduo huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri damu, kusababisha kufanyika kwa methemoglobini.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 245°C
Kiwango myeyuko: 63-64°C
Uzito wiani: 1.57 g/cm³
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 25°C: <1
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 5.6
Kiwango cha kumweka: 115°C
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 2.78
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005