DICAMBA ICSC: 0139
Aprili 1994

3,6-Dichloro-o-anisic acid
3,6-Dichloro-2-methoxybenzoic acid
CAS # 1918-00-9 C8H6Cl2O3
RTECS # DG7525000 Masi ya molekuli: 221.0
UN # 2769
EC # 607-043-00-X
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Michanganyiko ya vioevu vyenye vimumunyisho vya kaboni huweza kuwaka (moto). Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Hatari ya moto na mlipuko ikiwa michanganyiko vyenye vimumunyisho huweza kuwaka/kulipuka.


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MFIDUO KWA VIJANA NA WATOTO!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kupumua kwa shida. Kutapika. Udhaifu.
Uingizaji hewa (iwapo si poda).
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu. Maumivu. Kiwaa.
Miwanivuli ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: Xn
R: 22-41-52/53
S: (2-)-26-61
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61G53
Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Uingizaji hewa kwenye sakafu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
DICAMBA ICSC: 0139
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE ISO RANGI

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu na babuzi kama vile kloridi hidrojeni (tazama ICSC 0163).

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru hautafikiwa au utafikiwa polepole sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C; wakati wa kunyunyiza au kutawanya, hata hivyo, kwa kasi zaidi.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Hutengana chini ya kiwango mchemko ifikapo 200°C
Kiwango myeyuko: 114-116°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.57
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 25°C: 0.79
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 25°C: 0.0045
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 7.64
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 2.21
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Kama kiuadudu kiko kwa aina ya haidrokabonili kimumunyishaji, kutapika hakuwesi kusababishwa. Vimumunyishaji chukuzi vitumikavyo katika misombo ya kibiashara vyaweza kubadilisha tabia za kimaumbile na za kitoksini. Banvel, Banex, Dianat, Fallowmaster, Mediben, Metambane, Tracker, Trooper and Velsicol ni majina ya kibiashara. Angalia pia kadi ya viyeyusho endapo vimetumiwa kutengenezea dutu hii.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005