CYANOGEN BROMIDE ICSC: 0136
Aprili 2000

Bromine cyanide
Cyanobromide
Bromocyan
CAS # 506-68-3 BrCN
RTECS # GT2100000 Masi ya molekuli: 105.9
UN # 1889
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki lakini inapokanzwa hutengeneza gesi inayoungua. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kuumwa koo. Kikohozi. Mchomo. Degedege. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kukosa pumzi. Kupumua kwa shida. Kichefuchefu. Kupoteza fahamu. Kutapika.
Mfumo funge na uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. Maumivu. Malengelenge. (Tazama Kuvuta pumzi).
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Mpeleke kwa daktari. Tazama Vidokezo. Sukutua kinywa. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!).
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Zoa dutu iliyomwagika katika vyombo vinavyokalafatika. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Kisichoingiza hewa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Jasara tanzu za UN: 8
Kikundi Ufungashaji cha UN: I
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GTC2-I
Msimbo wa NFPA : H 3; F 0; R 1;
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Tazama Hatari za Kikemikali. Kavu. Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
CYANOGEN BROMIDE ICSC: 0136
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE ISO RANGI AU NYEUPE, YENYE HARUFU KALI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa na inapogusana na asidi, huzalisha gesi zenye sumu na ziwakazo, sianidi hidrojeni (tazama ICSC 0492) na gesi babuzi bromidi hidrojeni (tazama ICSC 0282). Humenyuka ikiwa na vioksidishaji vikali. Humenyuka polepole na maji na unyevuunyevu kufanyiza bromidi hidrojeni na sianidi hidrojeni. Hushambulia metali nyingi iwapo kuna maji.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera sana macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi ya mvuke wake kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Athari zinaweza kuchelewa. Dutu hii huweza kuathiri respiresheni ya seli, kusababisha degedege, kuzirai, kupoteza fahamu na kutoweza kupumua. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. Mfiduo huweza kusababisha kifo.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 61-62°C
Kiwango myeyuko: 52°C
Uzito wiani: 2.0 g/cm³
Umumunyifu katika maji: mmenyuko polepole
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 25°C: 16.2
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.6
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.53
DATA YA MAZINGIRA
Inashauriwa sana kutoruhusu kemikali hii iingie kwenye mazingira.
VIDOKEZO
Hujisablimisha kwenye joto la kawaida. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya mnyunyuzio mwafaka unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. Mazao ya kibiashara yaweza kuwa na vimumunyishaji vya klorofomi. Madhara kwa mazingira ya mkabala na dutu hii hayajachunguzwa.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005