| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua mno. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
Funga ugavi; kama haiwezekani na hakuna hatari kwa mazingira, acha moto uwake hadi ujizime; ama sivyo zima kwa kutumia poda, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Michanganyiko ya gesi/hewa hulipuka.
|
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. Zuia mlimbiko wa chaji za umemetuamo (k.m. kwa kutuliza) ikiwa ni kioevu. Tumia vifaa vya mkono visivyotoa cheche.
|
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kizunguzungu. Mazimbwezimbwe. Kuumwa kichwa. Msokoto wa tumbo.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
|
Glavu za kuhami baridi. Mavazi ya kinga.
|
UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Kiwaa.
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. (Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu). Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
|
Silinda maalum isiyopitisha joto na yenye zana maalum. Ainisho ya EU Alama: F+, Xn R: 12-40-52/53 S: (2-)-9-16-33-36/37-61 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 2.1 | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 20S1037 au 20G2F Msimbo wa NFPA : H 2; F 4; R 0; |
Isodhurika kwa moto.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: GESI OEVU ILIYOBANWA ISO RANGI, YENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI KWA MWILI: Gesi hii ni nzito kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapokanzwa au inapochomwa huzalisha gesi zenye sumu (kloridi hidrojeni - tazama ICSC 0163, fosjini - tazama ICSC 0007). VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 100 ppm kama TWA; (ngozi); A3; (ACGIH 2004). MAK: kuingia kupitia kwa ngozi (H); Aina ya sarakani: 3B; (DFG 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii mildlyinakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Uvukizaji wa haraka wa kioevu huweza kusababisha jamidi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva. Mfiduo juu zaidi ya OELhuweza kuleta kuzirai, kupoteza fahamu, kukosekana urari wa mapigo ya moyo na kifo. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 12.5°C Kiwango myeyuko: -138°C Uzito wiani (maji = 1): 0.918 Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 0.574 Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 133.3 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.22 |
Kiwango cha kumweka: -50°C c.c. Jotoridi la kujiwasha: 519°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 3.6-14.8 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.54 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Matumizi ya vileo huongeza athari zinazodhuru. Suuza nguo zilizosibikwa (hatari ya moto) kwa maji mengi. Usitumie karibu na moto au uso moto, au wakati wa kulehemu. Pindua silinda ivujayo ili mvujio uwe juu kuzuia gesi isitoke katika hali ya uoevu.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||