2-CHLOROANILINE ICSC: 0129
Aprili 2000

2-Chloroaminobenzene
1-Amino-2-chlorobenzene
Fast yellow GC base
o-Chloroaniline
CAS # 95-51-2 C6H6ClN / (C6H4)Cl(NH2)
RTECS # BX0525000 Masi ya molekuli: 127.6
UN # 2019
EC # 612-010-00-8
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Poda, AFFF, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU!

Kuvuta pumzi Midomo au kucha kugeuka kuwa bluu. Ngozi kugeuka kuwa bluu. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kukosa pumzi. Kichefuchefu. Kutapika. Degedege. Udhaifu. Kuchanganyikiwa. Kupoteza fahamu.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! (Tazama Kuvuta pumzi).
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, au kingao cha uso.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: T, N
R: 23/24/25-33-50/53
S: (1/2-)-28-36/37-45-60-61
Angalia: [C]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61S2019
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Weka gizani. Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
2-CHLOROANILINE ICSC: 0129
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI HADI MANJANO, CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HUGEUKA GIZA INAPOFIDULIWA NA HEWA.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu kama vile oksidi za nitrojeni, kloridi hidrojeni.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: BEI imetolewa; (ACGIH 2004).
MAK: IIb (thamani ya MAK bado haijapatikana lakini hati kamili ipo) kuingia kupitia kwa ngozi (H); (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho. Dutu hii huweza kuathiri damu, kusababisha kufanyika kwa methemoglobini. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. Athari zinaweza kuchelewa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri damu, kusababisha kufanyika kwa methemoglobini.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 209°C
Kiwango myeyuko: -2°C
Uzito wiani: 1.213 g/cm³
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 0.5
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 50
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.41
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.00
Kiwango cha kumweka: 108°C
Jotoridi la kujiwasha: >500°C
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.92
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Ina vizuiaji: 0.1% Hydrazine hydrate. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005