| |||||||||||||
| |||||||||||||
|
|||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Haiwaki lakini huongeza mwako wa dutu nyingine. Mimenyuko mingi yaweza kusababisha moto au kulipuka.
|
Usigusishe na vinavyoweza kuwaka.
|
Moto unapotokea katika eneo: maji mengi, mnyunyizio wa maji.
|
| MLIPUKO |
Hatari ya moto na mlipuko: tazama Hatari za Kikemikali.
|
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. USIACHE kikaathiriwa na msuguano au mshtuko.
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
|
| MFIDUO |
|
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kuumwa kichwa. Kupumua kwa shida. Kichefuchefu. Kukosa pumzi. Kuumwa koo. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
|
Mfumo funge na uingizaji hewa.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Wekundu. Maumivu.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Kwanza suuza kwa maji mengi, halafu vua nguo zilizosibikwa na suuza tena. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
|
|
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Ondoa gesi kwa mnyunyuzio mwembamba wa maji. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Ainisho ya EU Alama: O, T+, N R: 6-8-26-34-50 S: (1/2-)-23-26-28-36/37/39-38-45-61 Ainisho ya UN | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
|
Isodhurika kwa moto iwapo ndani ya jengo. Kinachotenganishwa na dutu zenye kuungua na za kunakisi. Baridi. Weka gizani. Uingizaji hewa kwenye sakafu.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: GESI NYEKUNDU-MANJANO, YENYE HARUFU KALI. HATARI KWA MWILI: Gesi hii ni nzito kuliko hewa. HATARI ZA KIKEMIKALI: Huweza kulipuka wakati wa kukanza, inapoathiriwa na mwanga au mishtuko au cheche. Dutu hii ni kioksidishaji madhubuti na humenyuka kwa ukali sana iwapo na maunzi yanayoweza kuwaka na yanayonakisi. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vikaboni, fosforasi, hidroksidi potasiamu na sulfuri, kusababisha athari ya moto na mlipuko. Humenyuka pamoja na maji huzalisha asidi hidrokloriki na asidi kloriki. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 0.1 ppm kama TWA, 0.3 ppm kama STEL; (ACGIH 2004). MAK: 0.1 ppm, 0.28 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: I(1); Kundi la waja wazito lililo hatarini: IIc; (DFG 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera kwa ukali macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Mfiduo zaidi ya OEL huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Dutu hii huweza kuathiri mapafu, kusababisha wa mapafu wa muda mrefu (chronic bronchitis). | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 11°C Kiwango myeyuko: -59°C Uzito wiani (maji = 1): 1.6 ifikapo 0°C (kioevu) Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 0.8 Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 101 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.3 |
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: zaidi ya 10 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa viumbe hai vya majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya mnyunyuzio mwafaka unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. Suuza nguo zilizosibikwa (hatari ya moto) kwa maji mengi.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||