| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Haiwaki lakini huongeza mwako wa dutu nyingine. Mimenyuko mingi yaweza kusababisha moto au kulipuka.
|
Usigusishe na vinavyoweza kuwaka, asetilini, ethilini, hidrojeni, amonia na metali laini.
|
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
|
| MLIPUKO |
Hatari ya moto na mlipuko inapogusana na dutu za kuwaka, amonia na metali laini.
|
|
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji BILA (vilivyomo) kugusa maji.
|
| MFIDUO |
|
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Inababua. Mchomo. Kukosa pumzi. Kikohozi. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kizunguzungu. Kupumua kwa shida. Kuumwa koo. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
|
Kinga ya kupumulia. Mfumo funge na uingizaji hewa.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI. Inababua. Mibabuko ya ngozi. Maumivu.
|
Glavu za kuhami baridi. Mavazi ya kinga.
|
Kwanza suuza kwa maji mengi, halafu vua nguo zilizosibikwa na suuza tena. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Inababua. Maumivu. Kiwaa. Kuungua kunakopenya sana.
|
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
|
|
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. KAMWE usielekeze nyiri ya maji juu ya kioevu. Ondoa gesi kwa mnyunyuzio mwembamba wa maji. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu). Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
|
Silinda maalum isiyopitisha joto. Kichafuzi cha maji/bahari. Ainisho ya EU Alama: T, N R: 23-36/37/38-50 S: (1/2-)-9-45-61 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 2.3 Jasara tanzu za UN: 8 | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 20S1017 Msimbo wa NFPA : H 4; F 0; R 0; OX |
Kinachotenganishwa na besi kali, dutu zenye kuungua na za kunakisi. Baridi. Kavu. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: GESI KIJANI-MANJANO, YENYE HARUFU KALI. HATARI KWA MWILI: Gesi hii ni nzito kuliko hewa. HATARI ZA KIKEMIKALI: Mmumunyo katika maji ni asidi kali humenyuka vikali ikiwa na besi na husababisha ulikaji. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na misombo kikaboni mingi, amonia, hidrojeni na metali laini kusababisha athari ya moto na mlipuko. Hushambulia metali nyingi iwapo kuna maji. Hushambulia plastiki, mpira na mipako. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 0.5 ppm kama TWA; 1 ppm kama STEL; A4; (ACGIH 2004). MAK: 0.5 ppm, 1.5 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: I(1); Kundi la waja wazito lililo hatarini: C; (DFG 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Inayotoza machozi. Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi ya gesi kunaweza kusababisha kichomi na kuvimba kwa mapafu kuathiri njia za hewa sizifanye kazi vizuri (RADS) (tazama Vidokezo). Uvukizaji wa haraka wa kioevu huweza kusababisha jamidi. Mfiduo juu zaidi ya OEL huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Dutu hii huweza kuathiri mapafu kusababisha ukamba wa mda mrefu. Dutu hii huweza mmunyo wa meno. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: -34°C Kiwango myeyuko: -101°C Uzito wiani (maji = 1): 1.4 ifikapo 20°C, 6.86 atm (kioevu) Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 0.7 Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 673 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.5 |
|||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya mnyunyuzio mwafaka unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi. Usitumie karibu na moto au uso moto, au wakati wa kulehemu. Usinyunyizie maji juu ya silinda inayovuja (kuzuia ulikaji wa silinda). Pindua silinda ivujayo ili mvujio uwe juu kuzuia gesi isitoke katika hali ya uoevu.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||