CADMIUM CHLORIDE ICSC: 0116
Aprili 2005

Cadmium dichloride
CAS # 10108-64-2 CdCl2
RTECS # EV0175000 Masi ya molekuli: 183.3
UN # 2570
EC # 048-008-00-3
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kikohozi. Kupumua kwa shida. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
Mfumo funge na uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama au au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Mchomo. Kuhara. Kichefuchefu. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kinga ya ziada ya binafsi: vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vinavyokalafatika; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama.
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi kikali cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: T+, N
R: 45-46-60-61-25-26-28-48/23/25-50/53
S: 53-45-60-61
Angalia: [E]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GT5-III
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, vyakula na malisho. Kavu. Kilichofungwa vizuri. Hifadhi mahali pasipokuwa na unyevu au uchafu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
CADMIUM CHLORIDE ICSC: 0116
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE ISO HARUFU, ZISIO NA RANGI, ZA RISHAI

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu kali: kadmiamu na klorini. Humenyuka pamoja na vioksidishaji vikali kusababisha mafusho yenye sumu ya klorini.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: (kama Cd) (vumbi) 0.01 mg/m³; (sehemu pumuzi) 0.002 mg/m³; kama TWA; A2 BEI imetolewa; (ACGIH 2005).
MAK: kuingia kupitia kwa ngozi (H) Aina ya sarakani: 1; Aina inayoleta mabadiliko kwa seli za uzazi: 3A; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Kikolezo cha chembechembeya dhuru yaweza kufikiwa haraka ikitawanywa hasa kama poda.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera kwa ukali irritating to macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii inakera kwa ukali njia ya utumbo. Kuvuta pumzi ya erosoli kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Mfiduo juu ya OEL huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri mafigo na mapafu kusababisha kuharibika kwa figo na vidonda vya tishu. Dutu hii husababisha kansa kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 960°C
Kiwango myeyuko: 568°C
Uzito wiani: 4.1 g/cm³
Umumunyifu katika maji: vizuri
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini. Kuzidisha kwa kemikali yaweza kutokea kwa mimea. Inashauriwa sana kutoruhusu kemikali hii iingie kwenye mazingira.
VIDOKEZO
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Usichukue nguo za kazi nyumbani. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya matibabu ya kuvuta hewa unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005