1-BUTANOL ICSC: 0111
Aprili 2005

n-Butanol
n-Butyl alcohol
Propyl carbinol
Butan-1-ol
Butyl alcohol
CAS # 71-36-3 C4H10O / CH3(CH2)3OH
RTECS # EO1400000 Masi ya molekuli: 74.1
UN # 1120
EC # 603-004-00-6
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 29°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 29°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO


Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo. Kuumwa kichwa. Kizunguzungu. Kusinzia.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi Wekundu. Maumivu. Ngozi kavu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kusinzia. Kizunguzungu. Kichefuchefu. Kuhara. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni. Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Osha salio kwa maji mengi.
Ainisho ya EU
Alama: Xn
R: 10-22-37/38-41-67
S: (2-)-7/9-13-26-37/39-46
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30S1120-III
Msimbo wa NFPA: H 1; F 3; R 0;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, alumini.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
1-BUTANOL ICSC: 0111
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Humenyuka pamoja na alumini inapokanzwa hadi 100°C, vioksidishaji vikali, kama vile trioksidi kromiamu, kutoa gesi inayoweza kuwaka/kulipuka (hidrojeni - tazama ICSC0001) Hushambulia aina fulani za plastiki, mpira na mipako.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 20 ppm kama TWA; (ACGIH 2005).
MAK: 100 ppm, 310 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: I(1); Kundi la waja wazito lililo hatarini: C; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru waweza kufikiwa polepole kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera ngozi, na inakera kwa ukali macho. Mvuke huu inakera macho na njia ya upumuaji Mfiduo juu ya OEL husababisha kupungua fahamu. Kumeza kioevu hiki kunaweza kusababisha madhara kwenye mapafu kukifyonza na kunaweza kuleta kichomi kinachotokana na kemikali.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Kioevu hukausha ngozi.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 117°C
Kiwango myeyuko: -90°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.81
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 7.7
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 0.58
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.6
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.01
Kiwango cha kumweka: 29°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 345°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.4-11.3
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.9
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO

MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005