METHYL BROMIDE ICSC: 0109
Aprili 1994

Bromomethane
Monobromomethane
(silinda)
CAS # 74-83-9 CH3Br
RTECS # PA4900000 Masi ya molekuli: 94.9
UN # 1062
EC # 602-002-00-2
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka katika hali mahususi. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto. Usigusishe na alumini, zinki, magnesiamu au oksijeni halisi.
Funga ugavi; kama haiwezekani na hakuna hatari kwa mazingira, acha moto uwake hadi ujizime. Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO Hatari ya moto na mlipuko inapogusana na alumini, zinki au magnesiamu.

Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU! EPUKA MFIDUO KWA VIJANA NA WATOTO!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Maumivu ya tumbo. Degedege. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kupumua kwa shida. Kutapika. Udhaifu. Kuona vitu visivyokuwepo. Kushindwa kusema. Kuduwaa.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Mnyeo. Kuwasha. Wekundu. Mchomo. Maumivu. Malengelenge. INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Glavu za kuhami baridi. Mavazi ya kinga.
UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu. Kiwaa. Muda wa upofu.
Miwanivuli ya usalama, kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza


KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. KAMWE usielekeze nyiri ya maji juu ya kioevu. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Ainisho ya EU
Alama: T, N
R: 23/25-36/37/38-48/20-50-59-68
S: (1/2-)-15-27-36/39-38-45-59-61
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 2.3

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 20S1062
Msimbo wa NFPA : H 3; F 1; R 0;
Isodhurika kwa moto iwapo ndani ya jengo. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, alumini na silinda yenye oksijeni. Baridi. Uingizaji hewa kwenye sakafu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
METHYL BROMIDE ICSC: 0109
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
GESI OEVU ILIYOBANWA ISO HARUFU NA ISO RANGI

HATARI KWA MWILI:
Gesi hii ni nzito kuliko hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa na inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu na babuzi kama vile bromidi hidrojeni, bromini na oksibromidi kaboni. Humenyuka ikiwa na vioksidishaji vikali. Hushambulia metali nyingi iwapo kuna maji. Husambulia alumini, zinki na magnesiamu kufanyiza misombo ya pairoforic kusababisha athari ya moto na mlipuko.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 1 ppm kama TWA; (ngozi); A4 (haijaainishwa kama kasinojeni kwa binadamu); (ACGIH 2004).
MAK: kunyonywa na ngozi (H); Aina ya sarakani: 3B; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kupitia katika ngozi, pia kama mvuke!

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi yenye dutu hii kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Uvukizaji wa haraka wa kioevu huweza kusababisha jamidi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva, mafigo na mapafu. Mfiduo wa viwango vya juu huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa neva, mafigo, moyo, ini na mapafu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 4°C
Kiwango myeyuko: -94°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.7
Umumunyifu katika maji, ml/100 ml ifikapo 20°C: 1.5
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.3
Jotoridi la kujiwasha: 537°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 10-16
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.19
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa samaki, mamalia, mimea, viumbe viishivyo ardhini.
VIDOKEZO
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika.Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu.Matumizi ajilani ya mnyunyuzio mwafaka unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika.Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi.Pindua silinda ivujayo ili mvujio uwe juu kuzuia gesi isitoke katika hali ya uoevu.Bromo-O-gas, Dowfume, Embafume, Halon 1001, Haltox, Meth-o-gas, Terabol na Terr-o-Gas 100 ni majina ya kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005