BIPHENYL ICSC: 0106
Aprili 1994

Diphenyl
Phenylbenzene
Dibenzene
CAS # 92-52-4 C12H10 / C6H5C6H5
RTECS # DU8050000 Masi ya molekuli: 154.2
UN # 3077
EC # 601-042-00-8
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka.
Usiwashe moto.
Mnyunyizo wa maji, poda, AFFF, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Chembechembe zilizotawanyika hufanya mchanganyiko ulipukao hewani.
Zuia utuaji wa vumbi; mfumo funge, vifaa vya umeme na taa visivyolipuka kwa vumbi. Zuia mlimbiko wa chaji za umemetuamo (k.m. kwa kutuliza).

MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kichefuchefu. Kutapika.
Epuka kuvuta pumzi yenye vumbi laini au ukungu. Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vinavyokalafatika; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio A/P2 cha mvuke kikaboni na vumbi linalodhuru). Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: Xi, N
R: 36/37/38-50/53
S: (2-)-23-60-61
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 9
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 90GM7-III
Msimbo wa NFPA : H 2; F 1; R 0;
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho, vioksidishaji.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
BIPHENYL ICSC: 0106
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE NYEUPE AU MAGAMBA , YENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Mlipuko wa vumbi huweza kutokea iwapo katika umbo la poda au punjepunje, vikichanganywa na hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Humenyuka pamoja na vioksidishaji.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 0.2 ppm kama TWA; (ACGIH 2004).
MAK: kuingia kupitia kwa ngozi (H); Aina ya sarakani: 3B; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho na njia ya upumuaji.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri ini na mfumo wa neva kusababisha kuharibika kwa utendaji.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 256°C
Kiwango myeyuko: 70°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.04
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 71°C: 133
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 5.3
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.0
Kiwango cha kumweka: 113°C c.c
Jotoridi la kujiwasha: 540°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 0.6 (ifikapo 111°C) - 5.8 (ifikapo 166°C)
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 3.16/4.09
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa maji. Katika mfuatano wa ulishano ambao ni muhimu kwa binadamu, mlimbikizo wa kibiliolojia hutokea, hasa kwenye mimea. Inashauriwa sana kutoruhusu kemikali hii iingie kwenye mazingira kwa sababu hubakia kwenye mazingira.
VIDOKEZO
Usichukue nguo za kazi nyumbani. Dowtherm A ni jina la kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005