BENZOTRICHLORIDE ICSC: 0105
Machi 1995

alpha,alpha,alpha-Trichlorotoluene
Trichlorophenylmethane
Phenylchloroform
(Trichloromethyl)benzene
CAS # 98-07-7 C7H5Cl3 / C6H5CCl3
RTECS # XT9275000 Masi ya molekuli: 195.48
UN # 2226
EC # 602-038-00-9
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto. Usigusishe na nyuso za moto.
Poda kavu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO

Utokeapo moto: poza mapipa n.k. kwa kunyunyizia maji BILA (vilivyomo) kugusa maji.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kikohozi. Kukosa pumzi. Kuumwa koo. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
Mfumo funge na uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Mchomo.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
Miwanivuli ya usalama, kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga mkavu au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Kisichoingiza hewa. Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: T
R: 45-22-23-37/38-41
S: 53-45
Angalia: [E]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 8
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 80S2226
Msimbo wa NFPA: H 3; F 1; R 0;
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho na maunzi yasiokubaliana. Tazama Hatari za Kikemikali. Kavu. Kilichofungwa vizuri. Uingizaji hewa kwenye sakafu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
BENZOTRICHLORIDE ICSC: 0105
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI HADI MANJANO-KAHAWIA, KIFUKACHO, KINATACHO CHENYE HARUFU KALI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa ,inapogusana na asidi na/au maji, huzalisha gesi zenye sumu na babuzi kama vile kloridi hidrojeni na asidi benzoiki. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji vikali, metali (hasa chuma), metali za alkali na metaliardhi ya alkali, besi na vikaboni kusababisha athari ya moto na mlipuko. Inapogusana na hewa hutoa kloridi hidrojeni yenye sumu na babuzi (tazama ICSC 0163. Hushambulia metali nyingi iwapo kuna maji. Hushambulia plastiki nyingi.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 0.1 ppm kama TWA; (ngozi); A2; (ACGIH 2004).
MAK: kuingia kupitia kwa ngozi (H); Aina ya sarakani: 2; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera inakera kwa ukalingozi na njia ya upumuaji na husababisha ulikaji kwa macho. Kuvuta pumzi wenye mvuke kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Kumeza kioevu hiki kunaweza kusababisha madhara kwenye mapafu kukifyonza na kunaweza kuleta kichomi kinachotokana na kemikali.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri ini, mafigo, tezi thioridi, mfumo mkuu wa neva na mfumo wa damu kusababisha kuharibika kwa utendaji na anemia. Dutu hii huenda inasababisha kansa kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 221°C
Kiwango myeyuko: -5°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.38
Umumunyifu katika maji: mmenyuko polepole
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 20
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 6.77
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.00
Kiwango cha kumweka: 108°C
Jotoridi la kujiwasha: 211°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 2.1-6.5 ifikapo 160°C
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 2.92
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Mvuke unaowaka / hewa mahuluti vigumu kuwasha, huweza kupatikana katika hali fulani. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya matibabu ya kuvuta hewa unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. Usichukue nguo za kazi nyumbani. Usitumie karibu na moto au uso moto, au wakati wa kulehemu.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005