BENZAL CHLORIDE ICSC: 0101
Aprili 2000

Dichloromethyl benzene
Benzylidene chloride
alpha, alpha-Dichlorotoluene
Benzyl dichloride
CAS # 98-87-3 C7H6Cl2 / C6H5CHCl2
RTECS # CZ5075000 Masi ya molekuli: 161.03
UN # 1886
EC # 602-058-00-8
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Poda, mnyunyizo wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO

Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kupumua kwa shida. Kuumwa koo.
Uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Maumivu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Kingao cha uso.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Mchomo. (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: T
R: 22-23-37/38-40-41
S: (1/2-)-36/37-38-45
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61S1886
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Tazama Hatari za Kikemikali. Uingizaji hewa kwenye sakafu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
BENZAL CHLORIDE ICSC: 0101
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI, CHENYE HARUFU KALI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapochomwa au inapogusana na asidi na maji, huzalisha mafusho yenye sumu kama vile kloridi hidrojeni (tazama ICSC 0163). Humenyuka pamoja na vioksidishaji vikali.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki
MAK: kuingia kupitia kwa ngozi (H); Aina ya sarakani: 2; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru hautafikiwa au utafikiwa polepole sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera kwa ukali macho, ngozi na njia ya upumuaji.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huenda inasababisha kansa kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 205°C
Kiwango myeyuko: -17°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.26
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 35.4°C: 0.13
Kiwango cha kumweka: 93°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 525°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.1-11
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 3.22
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO

MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005