| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua sana. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara. Usigusishe na asidi.
|
Maji mengi, povu linalokinza alkoholi, poda kavu. USITUMIE dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka. Hatari ya moto na mlipuko inapogusana na asidi, vioksidishaji.
|
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. USITUMIE hewa iliyoshindiliwa kujaza, kutoa au kuchukua. Tumia vifaa vya mkono visivyotoa cheche.
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
|
| MFIDUO |
|
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kupumua kwa shida. Kichefuchefu. Kutapika. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. Mibabuko ya ngozi. Malengelenge.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Maumivu ya tumbo. Mchomo. Kutapika. Mshtuko au kuzimia. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Shauriana na mtaalam. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Alama: F, T+, N R: 45-46-11-26/27/28-34-51/53 S: 53-45-61 Angalia: [D; E] Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Jasara tanzu za UN: 3 Kikundi Ufungashaji cha UN: I | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GTF-1 Msimbo wa NFPA: H 3; F 3; R 3; |
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na asidi, vioksidishaji, vyakula na malisho. Kavu. Hifadhi iwapo tu imetulia.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU KALI. HATARI KWA MWILI: Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana. Mvuke huu huchanganyika vema na hewa, mchanganyiko unaolipuka hutokea kwa urahisi. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii huweza kupolimisha kwa kuathiriwa na asidi, vioksidishaji kwa athari ya moto au mlipuko. Inapowaka hutengeneza mafusho babuzi na yenye sumu kama vile oksidi za nitrojeni. Dutu hii ni besi kali ya kati. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 0.5 ppm (ngozi); A3; (ACGIH 2002). MAK: H; Aina ya sarakani: 2; Aina inayoleta mabadiliko kwa seli za uzazi: 3A; (DFG 2002). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Husababisha ubabuzi inapomezwa. Kuvuta pumzi wa mvuke wake kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva, mafigo na ini. Mfiduo juu zaidi ya OEL huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Dutu hii ina uwezekano wa kusababisha kansa kwa binadamu. Yaweza kusababisha dhuru aina ya jenetiki kwa mbegu ya uzazi wa binadamu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 56-57°C Kiwango myeyuko: -74°C Uzito wiani (maji = 1): 0.8 Umumunyifu katika maji: kuchanganyika Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 21.3 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 1.5 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.1 Kiwango cha kumweka: -11°C c.c. Jotoridi la kujiwasha: 322°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 3.3-55 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -0.36 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi. Mvuke wa ethyleneimine hauzuiliki na unaweza kutengeneza polima katika matundu au vizimio vya miali ya moto kuziba kwa matundu hufuatia. Usichukue nguo za kazi nyumbani.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||