ALLYL GLYCIDYL ETHER ICSC: 0096
Machi 1996

((2-Propenyloxy)methyl)oxirane
Allyl 2,3-epoxypropyl ether
1-(Allyloxy)-2,3-epoxypropane
CAS # 106-92-3 C6H10O2
RTECS # RR0875000 Masi ya molekuli: 114.2
UN # 2219
EC # 603-038-00-1
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Poda, AFFF, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 48°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 48°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!

Kuvuta pumzi Mchomo. Kusinzia. Mazimbwezimbwe. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kukosa pumzi. Kutapika.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Ngozi kavu. Wekundu. Maumivu. Malengelenge.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu. Kiwaa. Kuungua kunakopenya sana.
Miwanivuli ya usalama, au kingao cha uso.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Mchomo. Kusinzia. Mazimbwezimbwe. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Osha salio kwa maji mengi. (Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Ainisho ya EU
Alama: Xn
R: 10-20/22-37/38-40-41-43-52/53-62-68
S: (2-)-24/25-26-36/37/39-61
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Jasara tanzu za UN: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30S2219
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, besi kali, asidi kali. Baridi. Weka gizani.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ALLYL GLYCIDYL ETHER ICSC: 0096
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI, CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii huenda ikatengeneza peroksidi lipukaji. Dutu hii huweza kupolimisha mapena. Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha gesi zenye sumu. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji vikali, asidi na besi.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 1 ppm kama TWA; A4 (haijaainishwa kama kasinojeni kwa binadamu); (ACGIH 2004).
MAK: kunyonywa na ngozi (H); uhisishaji wa ngozi (Sh); Aina ya sarakani: 2; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kupitia katika ngozi, na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Hubabua. Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi ya mvuke wake kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Mfiduo mkali waweza kudidimiza utendaji wa mfumo mkuu wa neva. Mfiduo husababisha kupungua fahamu. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Huweza kusababisha uharibifu wa kijeni kwa binadamu. Husababisha sumu kali inayoathiri uzazi kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 154°C
Kiwango myeyuko: -100°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.97
Umumunyifu katika maji, g/100 ml: 14
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 25°C: 0.63
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.9
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.02
Kiwango cha kumweka: 48°C o.c.
Jotoridi la kujiwasha: tazama Vidokezo
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: tazama Vidokezo
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Jotoridi la kujiwasha haijulikani katika maandiko. Vikomo vya ulipukaji havijulikani katika maandiko, japokuwa dutu hii inaweza kuwaka na ina kiwango cha kumweka pungufu ya 61°C. Matumizi ya vileo huongeza athari zinazodhuru. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi. Kagua kama kuna peroksidi kabla ya kunereka; iwapo chanya fanya iwe salama.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005