ACRYLONITRILE ICSC: 0092
Machi 2001

Cyanoethylene
2-Propenenitrile
Vinyl cyanide
CAS # 107-13-1 C3H3N / CH2=CH-CN
RTECS # AT5250000 Masi ya molekuli: 53.1
UN # 1093
EC # 608-003-00-4
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua sana. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara. Usigusishe na besi kali na asidi kali.
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizo wa maji, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka. Hatari ya moto na mlipuko inapogusana na besi kali na asidi kali.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. Tumia vifaa vya mkono visivyotoa cheche.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kukosa pumzi. Kutapika. Udhaifu. Degedege. Kubanwa kifua.
Mfumo funge na uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu. Tazama Vidokezo.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. Maumivu. Malengelenge. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Kwanza suuza kwa maji mengi, halafu vua nguo zilizosibikwa na suuza tena. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kutapika. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vyenye mifuniko. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: F, T, N
R: 45-11-23/24/25-37/38-41-43-51/53
S: 9-16-53-45-61
Angalia: [D na E]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Jasara tanzu za UN: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: I
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30S1093
Msimbo wa NFPA : H 4; F 3; R 2;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, besi kali, vyakula na malisho. Baridi. Weka gizani. Uingizaji hewa kwenye sakafu. Hifadhi iwapo tu imetulia.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ACRYLONITRILE ICSC: 0092
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI AU MANJANO ISIYOKOZA, CHENYE HARUFU KALI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hupolimisha kutokana na kukanza au kwa kuathiriwa na mwanga na besi, kusababisha athari ya moto na mlipuko. Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu kama vile sianidi hidrojeni, oksidi za nitrojeni. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na asidi kali na vioksidishaji vikali. Hushambulia plastiki na mpira.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 2 ppm kama TWA; (ngozi); A3; (ACGIH 2004).
MAK: kuingia kupitia kwa ngozi (H); kuhisisha ngozi (Sh); Aina ya sarakani: 2; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii na mvuke huu inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva. Mfiduo juu zaidi ya OEL huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Tazama Vidokezo. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva na ini. Dutu hii ina uwezekano wa kusababisha kansa kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 77°C
Kiwango myeyuko: -84°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.8
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 7
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 11.0
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 1.8
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.05
Kiwango cha kumweka: -1°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 481°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 3.0-17.0
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.25
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Mgusano na dutu hii waweza kusababisha sianidi. Pia shauriana na ICSC ya chumvi za sianidi, kama 0671. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi. Suuza nguo zilizosibikwa (hatari ya moto) kwa maji mengi.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005