| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto.
|
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizo wa maji, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Chembechembe zilizotawanyika hufanya mchanganyiko ulipukao hewani.
|
Zuia utuaji wa vumbi; mfumo funge, vifaa vya umeme na taa visivyolipuka kwa vumbi.
|
|
| MFIDUO |
|
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kuumwa koo. Udhaifu.
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. Maumivu. (Tazama Kuvuta pumzi).
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Maumivu ya tumbo. Udhaifu.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Sukutua kinywa. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Shauriana na mtaalam. Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
|
Maunzi maalum. Ainisho ya EU Alama: T R: 45-46-20/21-25-36/38-43-48/23/24/25-62 S: 53-45 Angalia: [D, E] Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: III | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GT2-III Msimbo wa NFPA : H 3; F 2; R 2; |
Kinachotenganishwa na vioksidishaji. Baridi. Weka gizani. Kilichofungwa vizuri.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: FUWELE NYEUPE HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii huweza kupolimisha kwa ukali sana kutokana na kukanza zaidi ya 85°C au kwa kuathiriwa na mwanga na vioksidishaji. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 0.03 mg/m³ kama TWA; (ngozi); A3 (imethibitishwa kuwa kasinojeni kwa wanyama na haijulikana kama ina athari kwa wanadamu); (ACGIH 2004). MAK: kuingia kupitia kwa ngozi (H); Aina ya sarakani: 2; Aina inayoleta mabadiliko kwa seli za uzazi: 2; (DFG 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa neva, kusababisha kuharibika kwa mfumo wa neva wa pembeni. Dutu hii huenda inasababisha kansa kwa binadamu. Huweza kusababisha uharibifu wa kijeni unaorithika kwa binadamu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango myeyuko: 84.5°C Uzito wiani: 1.13 g/cm³ Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 25°C: 204 Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 1 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.45 |
Kiwango cha kumweka: 138°C c.c. Jotoridi la kujiwasha: 424°C Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -1.65 - -0.67 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa samaki.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Usichukue nguo za kazi nyumbani.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||