| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua mno.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
Funga ugavi; kama haiwezekani na hakuna hatari kwa mazingira, acha moto uwake hadi ujizime; ama sivyo zima kwa kutumia poda, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Michanganyiko ya gesi/hewa hulipuka.
|
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. Zuia mlimbiko wa chaji za umemetuamo (k.m. kwa kutuliza). Tumia vifaa vya mkono visivyotoa cheche. Kwa kuzuia moto kuingia kwenye silinda tumia vizimio vya miali ya moto.
|
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kizunguzungu. Mazimbwezimbwe. Kuumwa kichwa. Msongo wa hewa.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
|
|
|
| Macho |
|
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu.
|
Silinda maalum isiyopitisha joto. Ainisho ya EU Alama: F+ R: 5-6-12 S: (2-)-9-16-33 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 2.1 | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 20S1001 Msimbo wa NFPA: H 1; F 4; R 3; |
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na - tazama Hatari za Kikemikali. Baridi.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: GESI ILIYOMUMUNYISHWA KATIKA ASETONI KUTOKANA NA SHINIKIZO, ISO RANGI HATARI KWA MWILI: Gesi hii huchanganyika vema na hewa, mchanganyiko unaolipuka hutokea kwa urahisi. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii huweza kupolimisha kutokana na kukanza. Dutu hugawanyika ikichomwa na ongezeko la kanieneo pamoja na moto na hatari ya mlipuko. Dutu hii ni kinakisishaji kikali na humenyuka kwa ukali sana ikiwa na vioksidishaji na ikiwa na florini au klorini inapoathiriwa na mwanga kusababisha athari ya moto na mlipuko. Humenyuka pamoja na shaba, fedha na zebaki au chumvi zake, kutoa misombo yenye wepesi wa mshitusho (asetilidi). VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: Kinacho nyima pumzi sahili, (ACGIH 2003). MAK haijathibitishwa. |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Isipodhibitiwa gesi hii huweza kusababisha kukosekana hewa kwa kupunguza kiasi cha oksijeni hewani katika maeneo funge. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Kinacho nyima pumuzi sahili. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: -85°C Kiwango myeyuko: -81°C Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 0.12 Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 4460 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 0.907 |
Kiwango cha kumweka: gesi iunguayo Jotoridi la kujiwasha: 305°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 2.5-100 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.37 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Bomba la gesi hii lisizidi kuwa na 63% ya shaba. Pima kiasi cha oksijeni kabla ya kuingia katika eneo. Baada ya kutumia katika kulehemu, funga valvu; kagua neli, mara kwa mara n.k., na chunguza uvujaji kwa kutumia maji na sabuni. Tokeo la tekinikali la weza kuwa na mchafuko unaoweza kugeusa matokeo kwa afya. Kwa maelezo zaidi ona ICSC0694 Fosfini.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||