| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua sana.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
Poda, povu linalokinza alkoholi, maji mengi, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka.
|
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. USITUMIE hewa iliyoshindiliwa kujaza, kutoa au kuchukua.
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kuchanganyikiwa. Kikohozi. Kizunguzungu. Kusinzia. Kuumwa kichwa. Kuumwa koo. Kupoteza fahamu.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Ngozi kavu.
|
Glavu za kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Kiwaa. Uwezekano wa kuharibu konea.
|
Miwani ya usalama, au kingao cha uso, lenzi mboni zilivaliwa.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Kichefuchefu. Kutapika. (zaidi tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Kisha osha kwa maji mengi. (Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Ainisho ya EU Alama: F, Xi R: 11-36-66-67 S: (2-)-9-16-26 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 3 Kikundi Ufungashaji cha UN: II | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30S1090 Msimbo wa NFPA : H 1; F 3; R 0; . |
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI KWA MWILI: Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana. HATARI ZA KIKEMIKALI: Inapogusana na vioksidishaji vikali kama vile asidi nitriki, peroksidi hidrojeni, dutu hii huweza kutengeneza peroksidi lipukaji. Humenyuka pamoja na klorofom na bromofom kukiwepo hali ya besi kusababisha athari ya moto na mlipuko. Hushambulia plastiki. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 500 ppm kama TWA, 750 ppm kama STEL; A4 (haijaainishwa kama kasinojeni kwa binadamu); BEI imetolewa; (ACGIH 2004). MAK: 500 ppm 1200 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: I(2); Kundi la waja wazito lililo hatarini: IIc; (DFG 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kupitia katika ngozi. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C; wakati wa kutawanya, hata hivyo, kwa kasi zaidi. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Mvuke huu inakera macho na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva, ini, mafigo na njia ya utumbo. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. Dutu hii huweza kuathiri damu na uboho. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 56°C Kiwango myeyuko: -95°C Uzito wiani (maji = 1): 0.8 Umumunyifu katika maji: kuchanganyika Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 24 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.0 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.2 Kiwango cha kumweka: -18°C c.c. Jotoridi la kujiwasha: 465°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 2.2-13 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -0.24 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Matumizi ya vileo huongeza athari zinazodhuru.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||