| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 32°C.
|
Mfumo funge wa zaidi ya 32°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka. Zuia mlimbiko wa chaji za umemetuamo (k.m. kwa kutuliza).
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU! EPUKA MFIDUO KWA WANAWAKE (WAJAWAZITO)!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kizunguzungu. Kusinzia. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Ngozi kavu. Wekundu.
|
Glavu za kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Miwani ya usalama.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Mchomo. Maumivu ya tumbo. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Uingizaji hewa. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni).
|
Ainisho ya EU Alama: Xn R: 10-20/21-38 S: (2-)-25 Angalia: [C] Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 3 Kikundi Ufungashaji cha UN: III | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30S1307-III Msimbo wa NFPA: H 2; F 3; R 0; |
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, na asidi kali.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI KWA MWILI: Kutokana na mtiririko, mchukucho n.k., chaji za kiumemetuamo huweza kutokea. HATARI ZA KIKEMIKALI: Humenyuka pamoja na asidi kali na vioksidishaji vikali. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 100 ppm kama TWA; 150 ppm kama STEL A4 (ACGIH 2001). BEI taja kwa (ACGIH 2001). EU OEL: 50 ppm kama TWA; 100 ppm kama STEL (ngozi) (EU 2000). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru waweza kufikiwa polepole kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho na ngozi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva. Kumeza kioevu hiki kunaweza kusababisha madhara kwenye mapafu kukifyonza na kunaweza kuleta kichomi kinachotokana na kemikali. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Kioevu hukausha ngozi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva. Mfiduo kwa dutu hii yaweza kuzidisha kutosikia kunausababishwa na kelele. Majaribio kwa wanyama yanaonyesha kuwa dutu hii huenda ikasababisha athari za sumu kwa uzazi na kukua kwa binadamu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 144°C Kiwango myeyuko: -25°C Uzito wiani (maji = 1): 0.88 Umumunyifu katika maji: hakuna Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 0.7 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.7 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.02 Kiwango cha kumweka: 32°C c.c. Jotoridi la kujiwasha: 463°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 0.9-6.7 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 3.12 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Mapendekezo kwenye kadi hii pia yanahusu zilini ya kiteknikali. Ona ICSC 0086 p-Xylene na 0085 m-Xylene.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||