VINYLIDENE CHLORIDE ICSC: 0083
Aprili 2000

1,1-Dichloroethene
1,1-Dichloroethylene
VDC
CAS # 75-35-4 C2H2Cl2 / H2C=CCl2
RTECS # KV9275000 Masi ya molekuli: 97
UN # 1303 (imezuiwa)
EC # 602-025-00-8
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua mno. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Poda, mnyunyizo wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. Tumia vifaa vya mkono visivyotoa cheche.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU!

Kuvuta pumzi Kizunguzungu. Kusinzia. Kupoteza fahamu.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Maumivu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kuumwa koo. (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Umpe maji mengi ya kunywa. Kupumzika.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Kisichoingiza hewa. Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Kichafuzi cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: F+, Xn
R: 12-20-40
S: (2-)-7-16-29-36/37-46
Angalia: [D]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: I
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30S1303
Msimbo wa NFPA : H 2; F 4; R 2;
Isodhurika kwa moto. Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Kinachotenganishwa na maunzi yasiokubaliana (tazama Hatari za Kikemikali). Baridi. Weka gizani. Hifadhi iwapo tu imetulia.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
VINYLIDENE CHLORIDE ICSC: 0083
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI VUKIVU, CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana. Mvuke wa kloridi vinilidini monoma hauzuiliki na unaweza kutengeneza polima katika matundu au vizimio vya miali ya moto vya matangi ya kuhifadhia, kuziba kwa matundu hufuatia.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii huweza kutengeneza peroksidi lipukaji kwa urahisi. Dutu hii hupolimisha kirahisi kutokana na kukanza au kwa kuathiriwa na oksijeni, mwanga, shaba au alumini kwa athari ya moto au mlipuko. Huweza kulipuka wakati wa kukanza au ikigusana na mialimoto. Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu na babuzi (kloridi hidrojeni, fosjini). Humenyuka kwa ukali sana ikiwa na vioksidishaji .

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 5 ppm kama TWA; A4; (ACGIH 2004).
MAK: 2 ppm, 8.0 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: II(2); Aina ya sarakani: 3B; Kundi la waja wazito lililo hatarini: C; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kumeza kioevu hiki kunaweza kusababisha madhara kwenye mapafu kukifyonza na kunaweza kuleta kichomi kinachotokana na kemikali. Mfiduo wa viwango vya juu husababisha kupungua fahamu.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. Dutu hii huweza kuathiri mafigo na ini.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 32°C
Kiwango myeyuko: -122°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.2
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 25°C: 0.25
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 66.5
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.3
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 2.5
Kiwango cha kumweka: -25°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 570°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 5.6-16
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.32
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Ongezeko la kiimarishaji au kiviza huweza kuathiri tabia ya kitoksini za dutu hii, shauriana na mtaalam. Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi. Usitumie karibu na moto au uso moto, au wakati wa kulehemu.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005