| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua mno. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
Funga ugavi; kama haiwezekani na hakuna hatari kwa mazingira, acha moto uwake hadi ujizime; ama sivyo zima kwa kutumia poda,dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Michanganyiko ya gesi/hewa hulipuka.
|
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. Tumia vifaa vya mkono visivyotoa cheche.
|
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
|
| MFIDUO |
|
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Kizunguzungu. Kusinzia. Kuumwa kichwa. Kupoteza fahamu.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
|
Glavu za kinga. Glavu za kuhami baridi. Mavazi ya kinga.
|
UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Ondoa vyanzo vyote vya moto. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Ainisho ya EU Alama: F+, T R: 45-12 S: 53-45 Angalia: [D] Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 2.1 | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 150 Msimbo wa NFPA : H 2; F 4; R 2; |
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na maunzi yasiokubaliana (tazama Hatari za Kikemikali). Baridi. Hifadhi iwapo tu imetulia.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: GESI OEVU ILIYOBANWA ISO RANGI, YENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI KWA MWILI: Gesi hii ni nzito kuliko hewa. na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana. Mvuke wa kloridi vinili monoma hauzuiliki na unaweza kutengeneza polima katika matundu au vizimio vya miali ya moto vya matangi ya kuhifadhia, kuziba kwa matundu hufuatia. HATARI ZA KIKEMIKALI: Katika hali mahsusi dutu hii huweza kutengeneza peroksidi na kuanzisha upolimishaji lipukaji. Dutu hii hupolimisha mapema kutokana na kukanza na kwa kuathiriwa na hewa, mwanga, na inapogusana na vichocheo, vioksidishaji vikali na metali kama vile shaba na alumini kwa athari ya moto au mlipuko. Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu na babuzi (kloridi hidrojeni, fosjini). Hushambulia feri na chuma iwapo kuna unyevuunyevu. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 1 ppm kama TWA; A1; (ACGIH 2004). MAK: Aina ya sarakani: 1; (DFG 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho. Kioevu hiki huweza kusababisha jamidi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva. Mfiduo husababisha kupungua fahamu. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Dutu hii huweza kuathiri wengu, damu na mishipa midogo ya damu, tishu na mifupa ya vidole vya mikono. Dutu hii husababisha kansa kwa binadamu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: -13°C Kiwango myeyuko: -154°C Uzito wiani (maji = 1): (kioevu) 0.9 Uzito wiani: (mvuke) at 15°C 8 g/l Umumunyifu katika maji: hakuna Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 343 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.2 |
Kiwango cha kumweka: -78°C c.c. Jotoridi la kujiwasha: 472°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 3.6-33 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.6 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa maji ya ardhini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi. Usitumie karibu na moto au uso moto, au wakati wa kulehemu. Ongezeko la kiimarishaji au kiviza huweza kuathiri tabia ya kitoksini za dutu hii, shauriana na mtaalam.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||