| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka katika hali mahususi. Tazama Vidokezo.
|
|
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
|
| MLIPUKO |
|
Zuia mlimbiko wa chaji za umemetuamo (k.m. kwa kutuliza).
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kizunguzungu. Kusinzia. Kuumwa kichwa. Udhaifu. Kichefuchefu. Kupoteza fahamu.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Ngozi kavu. Wekundu.
|
Glavu za kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Miwani ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Maumivu ya tumbo. (Tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Umpe maji mengi ya kunywa. Kupumzika.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni). Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari. Ainisho ya EU Alama: T R: 45-36/38-52/53-67 S: 53-45-61 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: III | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61S1710 Msimbo wa NFPA : H 2; F 1; R 0; |
Kinachotenganishwa na metali (tazama Hatari za Kikemikali), besi kali, vyakula na malisho. Kavu. Weka gizani. Uingizaji hewa kwenye sakafu.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI, CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI KWA MWILI: Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa. Kutokana na mtiririko, mchukucho n.k., chaji za kiumemetuamo huweza kutokea. HATARI ZA KIKEMIKALI: Inapogusana na nyuso zenye joto au mialimoto dutu hii hutengana na kutengeneza mafusho babuzi na yenye sumu (fosjini, kloridi hidrojeni). Dutu hii hutengana inapogusana na alkali kali huzalisha dikloroasetilini, ambayo huongeza athari ya moto. Humenyuka vikali ikiwa na poda ya metali kama vile magnesiamu, alumini, titaniamu na bariamu. Iliyovunjika polepole kwa mwanga huku unyevu ukiwepo pamoja na ufanyikaji wa asidi hidrokloriki yenye babuzi. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 50 ppm kama TWA; 100 ppm kama STEL; A5; BEI imetolewa; (ACGIH 2004). MAK: Aina ya sarakani: 1; Aina inayoleta mabadiliko kwa seli za uzazi: 3B; (DFG 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho na ngozi. Kumeza kioevu hiki kunaweza kusababisha madhara kwenye mapafu kukifyonza na kunaweza kuleta kichomi kinachotokana na kemikali. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva, kusababisha kutoweza kupumua. Mfiduo husababisha kupungua fahamu. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva, kusababisha kupungua fahamu. Dutu hii huweza kuathiri ini na mafigo (tazama Vidokezo). Dutu hii huenda inasababisha kansa kwa binadamu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 87°C Kiwango myeyuko: -73°C Uzito wiani (maji = 1): 1.5 Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 0.1 Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 7.8 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.5 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.3 Jotoridi la kujiwasha: 410°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 8-10.5 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 2.42 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii inaweza kusababisha madhara yatakayoonekana baadaye katika mazingira ya maji.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Mvuke unaowaka / hewa mahuluti vigumu kuwasha, huweza kupatikana katika hali fulani. Matumizi ya vileo huongeza athari zinazodhuru. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi. Usitumie karibu na moto au uso moto, au wakati wa kulehemu. Ongezeko la kiimarishaji au kiviza huweza kuathiri tabia ya kitoksini za dutu hii, shauriana na mtaalam.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||