| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka katika hali mahususi. Ukanzaji unaweza kusababisha ongezeko la kanieneo na kuleta athari ya kupasuka. Tazama Vidokezo.
|
Usiwashe moto. Usigusishe na nyuso za moto.
|
Poda, mnyunyizo wa maji, povu, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Tazama Vidokezo.
|
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kizunguzungu. Kusinzia. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kukosa pumzi. Kupoteza fahamu.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! Ngozi kavu.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
|
Miwani ya usalama, au kingao cha uso.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
(Tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Kichafuzi cha maji/bahari. Ainisho ya EU Alama: Xn R: 20/21/22-40-66 S: (2-)-9-36/37-46 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 9 Kikundi Ufungashaji cha UN: III | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 90GM6-III Msimbo wa NFPA : H 3; F 1; R 0; |
Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, besi kali, metali nyingi. Kilichofungwa vizuri. Uingizaji hewa kwenye sakafu.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI, CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI KWA MWILI: Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa. HATARI ZA KIKEMIKALI: Inapogusana na nyuso zenye joto au mialimoto dutu hii hutengana na kutengeneza kloridi hidrojeni (ICSC 0163), fosjini (ICSC 0007), na gesi nyinginezo zenye sumu. Humenyuka pamoja na vioksidishaji vikali, besi kali na metali kama vile sodiamu, potasiamu, magnesiamu na poda ya alumini. Hushambulia plastiki nyingi, mpira, chuma na zinki. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 10 ppm kama TWA; (ngozi); A3; (ACGIH 2004). MAK: 10 ppm, 55 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: II(2); kuingia kupitia kwa ngozi (H); Aina ya sarakani: 3B; (DFG 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva, mafigo, ini, kusababisha kuharibika kwa utendaji wa mfumo mkuu wa neva, kuharibika kwa ini na figo. Mfiduo wa viwango vya juu huweza kusababisha kupoteza fahamu. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Kioevu hukausha ngozi. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 114°C Kiwango myeyuko: -36°C Uzito wiani (maji = 1): 1.44 Umumunyifu katika maji: hakuna Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 2.5 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.6 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 4.6 Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 6-15.5 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 2.35 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kiwango cha kumweka haijulikani katika maandiko. Mvuke unaowaka / hewa mahuluti vigumu kuwasha, huweza kupatikana katika hali fulani. Matumizi ya vileo huongeza athari zinazodhuru. Uhusiano baina ya harufu na kikomo cha mfiduo wa kazi hauwezi kuonyeshwa. Usitumie karibu na moto au uso moto, au wakati wa kulehemu.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||