| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
|
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
|
| MLIPUKO |
|
|
|
| MFIDUO |
|
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
(Tazama Kumeza).
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! (Tazama Kumeza.)
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
|
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Maumivu ya tumbo. Kichefuchefu. Kutapika. Kuumwa kichwa. Udhaifu. Uchungu kwa miguu. Kutoona vizuri. Kupotea kwa nywele. Kutotulia. Degedege. Moyo kuenda haraka. Ona Vidokezo.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Zoa dutu iliyomwagika katika vyombo vinavyokalafatika. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P3 cha chembe zenye sumu).
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Alama: T+ R: 26/28-33-53 S: (1/2-)-13-28-45-61 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: I | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GT5-I
|
Kinachotenganishwa na asidi kali, florini, halojeni nyingine, vyakula na malisho.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: METALI BLUU-NYEUPE, LAINI SANA. HUGEUKA KIJIVU INAPOFIDULIWA NA HEWA. HATARI ZA KIKEMIKALI: Humenyuka pamoja na asidi kali. Humenyuka pamoja na florini na halojeni nyingine kwenye joto la kawaida. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 0.1 mg/m³ kama TWA (ngozi) (ACGIH 2001). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa hasa iwapo katika hali ya poda. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii huweza kuathiri njia ya utumbo, mfumo wa neva, mafigo na mfumo wa moyo na mishipa Yaweza kusababisha kupotea kwa nywele na kudhoufika kwa makucha. Inapomezwa mfiduo huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa moyo na mishipa, mfumo wa neva na yaweza kusababisha kupotea kwa nywele. Majaribio kwa wanyama yanaonyesha kuwa dutu hii huenda ikasababisha athari za sumu kwa uzazi na kukua kwa binadamu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 1457°C Kiwango myeyuko: 304°C Uzito wiani (maji = 1): 11.9 Umumunyifu katika maji: hakuna |
|||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini. Kuzidisha kwa kemikali yaweza kutokea kwa mfano kufuata mwishono wa vyakula kwa mboga na viumbe vya majini. Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa ndege na mamalia. Inashauriwa sana kutoruhusu kemikali hii iingie kwenye mazingira. Dutu hii inaweza kusababisha madhara yatakayoonekana baadaye katika mazingira ya maji.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Dalili ya madhara ya thaliamu kwa kawaida hutokea polepole; dalili kwa tumbo (kusikia kama kutapika, kutapika, uchungu kwa tumbo) hutokea kwa kawaida baada ya saa chache baada ya mfiduo, na kuhusu neva na dalili zingine yaweza kutokea baada ya siku 2-5. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Usichukue nguo za kazi nyumbani. Ona ICSC 0336 (Thallium sulfate), 1221 (Thallium carbonate).
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||