(2,4,5-TRICHLOROPHENOXY) ACETIC ACID ICSC: 0075
Aprili 2005

2,4,5-T
CAS # 93-76-5 C8H5Cl3O3 / C6H2Cl3OCH2COOH
RTECS # AJ8400000 Masi ya molekuli: 255.5
UN # 3345
EC # 607-041-00-9
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka katika hali mahususi. Michanganyiko ya vioevu vyenye vimumunyisho vya kaboni huweza kuwaka (moto). Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Mnyunyizo wa maji, poda.
MLIPUKO


MFIDUO Tazama Vidokezo.
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MFIDUO KWA WANAWAKE (WAJAWAZITO)!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Kuhara. Kusinzia. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru. Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vilivyofunikwa; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: Xn, N
R: 22-36/37/38-50/53
S: (2-)-24-60-61
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GT7-III
Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Hifadhi mahali pasipokuwa na unyevu au uchafu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
(2,4,5-TRICHLOROPHENOXY) ACETIC ACID ICSC: 0075
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
PODA FUWELE NYEUPE

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa na inapochomwa kuzalisha gesi zenye sumu na babuzi pamoja na fosjini (tazama ICSC0007) na kloridi hidrojeni (tazama ICSC0163). Mmumunyo huu katika maji ni asidi dhaifu.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 10 mg/m³ kama TWA; A4 (ACGIH 2005).
MAK: (kiwango cha kunuswa) 10 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: II(2); H Kundi la waja wazito lililo hatarini: C; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Kikolezo cha chembechembe ya dhuru yaweza kufikiwa haraka wakati wa kunyunyiza au inapotawanywa hasa iwapo katika hali ya poda.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho na njia ya upumuaji.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Majaribio kwa wanyama yanaonyesha kuwa dutu hii huenda ikasababisha athari za sumu kwa uzazi na kukua kwa binadamu. Tazama Vidokezo.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Hutengana kabla ya kuchemka
Kiwango myeyuko: 153-158°C
Uzito wiani: 1.80 g/cm³
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 25°C: 0.03
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 25°C: sio na maana
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 4
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii huingia katika mazingira kwa matumizi ya kawaida. Utaratibu wa hali ya juu lazima unahitajika ili kuzuia kiasi zaidi kisitokee kama kupitia kwa kutupwa ovyo.
VIDOKEZO
Jotoridi linalosababisha mtengano haijulikani katika maandiko. Mazao ya kibiashara yaweza kuwa na dioksini sumu yenye uwezo wa kusababisha madhara ya afya (chunusi, mabadiliko ya ini (tazama ICSC1467 2,3,7,8-TCDD). Angalia pia kadi ya viyeyusho endapo vimetumiwa kutengenezea dutu hii. Vimumunyishaji chukuzi vitumikavyo katika misombo ya kibiashara vyaweza kubadilisha tabia za kimaumbile na za kitoksini. Mapendekezo kwenye kadi hii pia yanahusu salts of 2,4,5-Trichlorophenoxyacetic acid.. Esterone 245, Trioxone na Weedone ni majina ya kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005