STYRENE ICSC: 0073
Aprili 1994

Vinylbenzene
Phenylethylene
Ethenylbenzene
CAS # 100-42-5 C8H8/C6H5CH=CH2
RTECS # WL3675000 Masi ya molekuli: 104.1
UN # 2055 (styrene monoma, imezuiwa)
EC # 601-026-00-0
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Poda, AFFF, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 31°C. Tazama Vidokezo.
Mfumo funge wa zaidi ya 31°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka. Zuia mlimbiko wa chaji ya mtuamo umeme (k.m. kwa kutuliza).
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!

Kuvuta pumzi Kizunguzungu. Kuzinzia. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Udhaifu.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi Wekundu.
Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. (Zaidi tazama Uvutaji pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Umpe maji mengi ya kunywa. Kupumzika.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Kisichoingiza hewa. Kichafuzi cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: Xn
R: 10-20-36/38
S: (2-)-23
Angalia: [D]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30S2055
Msimbo wa NFPA : H 2; F 3; R 2;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na maunzi yasiokubaliana (tazama Hatari za Kikemikali). Baridi. Weka gizani. Hifadhi iwapo tu imetulia.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
STYRENE ICSC: 0073
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI HADI MANJANO, CHA MAFUTA

HATARI KWA MWILI:
Kutokana na mtiririko, mchukucho n.k., chaji za kiumemetuamo huweza kutokea.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii huweza kutengeneza peroksidi lipukaji. Dutu hii huweza kupolimisha kutokana na kupata joto, kwa kuathiriwa na mwanga na inpogusana na misombo mingi kama vile oksijeni, vioksidishaji, peroksidi na asidi kali, kwa athari ya moto au mlipuko. Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu, oksidi styrene. Hushambulia shaba na aloi yake.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 50 ppm; 213 mg/m³ STEL: 100 ppm; 426 mg/m³ (ngozi) (ACGIH 1993-1994)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kupitia katika ngozi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru waweza kufikiwa polepole kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kumeza kioevu hiki kunaweza kusababisha madhara kwenye mapafu kukifyonza na kunaweza kuleta kichomi kinachotokana na kemikali. Mfiduo husababisha kupungua fahamu.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Kuvuta hewa kwa kurudia au muda mrefu huweza kusababisha pumu. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva. Dutu hii ina uwezekano wa kusababisha kansa kwa binadamu. Tazama Vidokezo.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 145°C
Kiwango myeyuko: -30.6°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.9
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 25°C: 0.03
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 0.7
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.6
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.02
Kiwango cha kumweka: 31°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 490°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 0.9-6.8
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 3.2
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Aghalabu dalili za pumu hazijitokezi mpaka baada ya saa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Kwa hiyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Mtu yeyote aliyeonyesha dalili za pumu kutokana na dutu hii kamwe asigusane na dutu hiyo tena. Ongezeko la kiimarishaji au kiviza huweza kuathiri tabia ya kitoksini za dutu hii, shauriana na mtaalam. Kagua kama kuna peroksidi kabla ya kunereka; iwapo chanya fanya iwe salama. Mvuke wa styrene monoma hauzuiliki na unaweza kutengeneza polima katika matundu au vizimio vya miali ya moto vya matangi ya kuhifadhia, kuziba kwa matundu hufuatia.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005