| |||||||||||||
| |||||||||||||
|
|||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto. Usigusishe na vioksidishaji.
|
Poda, AFFF, povu, dioksidi kaboni. USITUMIE maji.
|
| MLIPUKO |
Hatari ya moto na mlipuko inapogusana na vioksidishaji.
|
|
|
| MFIDUO |
|
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Muwasho puani. Kikohozi. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kupumua kwa shida. Kichefuchefu. Kuumwa koo. Kutapika. Udhaifu. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Wekundu. Mibabuko ya ngozi. Maumivu. Kubadilika rangi.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu. Vua nguo zilizosibikwa.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Kiwaa.
|
Miwani ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Ladha ya metali. Kuhara. Baridi kali. Homa. (zaidi tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P3 cha chembe zenye sumu).
|
Kisichoingiza hewa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Alama: T R: 23/25-33-53 S: (1/2-)-20/21-28-45-61 Ainisho ya UN | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
|
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, asidi kali, vyakula na malisho. Kavu.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: MANGO KATIKA MAUMBO MBALIMBALI, ISO HARUFU, MANGO AMOFASI NYEKUNDU-KAHAWIA HADI KIBLUU-NYEUSI AU FUWELE ANGAVU NYEKUNDU AU FUWELE KIJIVU KAMA METALI HADI NYEUSI. HATARI ZA KIKEMIKALI: Inapokanzwa, hutoa mafusho yenye sumu. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji na asidi kali. Humenyuka pamoja na maji kwenye 50°C kufanyiza gesi inayoweza kuwaka (hidrojeni ICSC 0001) na asidi seleniasi. Humenyuka kwa mwangazo ikikanzwa na fosforasi na metali kama vile nikeli, zinki, sodiamu, potasiamu, platinam. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 0.2 mg/m³ kama TWA; (ACGIH 2004). MAK: (kiwango cha kunuswa) 0.05 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: II(4); Aina ya sarakani: 3B; Kundi la waja wazito lililo hatarini: C; (DFG 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi yenye vumbi kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Kuvuta pumzi yenye mafusho kunaweza kusababisha dalili za kukosa hewa, jamidi na homa, na ugonjwa wa mapafu. Athari zinaweza kuchelewa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. Dutu hii huweza kuathiri njia ya upumuaji, njia ya utumbo, na ngozi kusababisha kichefuchefu, kutapika, kikohozi, ngozi kugeuka manjano, kutoka kucha, kupumua kwa maumivu na meno kuharibika. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 685°C Kiwango myeyuko: 170-217°C Uzito wiani (maji = 1): 4.8 Umumunyifu katika maji: hakuna Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 0.1 |
|||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Usichukue nguo za kazi nyumbani.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||