PHENOL ICSC: 0070
Oktoba 2001

Carbolic acid
Phenic acid
Hydroxybenzene
CAS # 108-95-2 C6H6O / C6H5OH
RTECS # SJ3325000 Masi ya molekuli: 94.1
UN # 1671
EC # 604-001-00-2
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka.
Usiwashe moto. Usigusishe na strong vioksidishaji.
Povu linalokinza alkoholi, poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 79°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 79°C, uingizaji hewa.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kuumwa koo. Mchomo. Kikohozi. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kutapika. Kukosa pumzi. Kupumua kwa shida. Kupoteza fahamu. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
Epuka kuvuta pumzi yenye vumbi laini au ukungu. Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Kunyonyowa kwa urahisi. Mibabuko nzito ya ngozi. Kuganda. Msukosuko. Kuzimia. Kukosa fahamu. Kifo.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Kwa kuondoa dutu hii tumia polyethilini glikoli 300 au mafuta yaliotokana na mimea. Mpeleke kwa matibabu. Vaa glavu za kinga unapotoa huduma ya kwanza.
Macho Maumivu. Wekundu. Upofu wa kudumu. Kuungua kunakopenya sana.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Inababua. Maumivu ya tumbo. Degedege. Kuhara. Mshtuko au kuzimia. Kuumwa koo. Unaokaribia kijani nzito na wenye mvuke.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vinavyokalafatika; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu). Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: T, C
R: 23/24/25-34-48/20/21/22-68
S: (1/2-)-24/25-26-28-36/37/39-45
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61S1671
Msimbo wa NFPA: H 3; F 2; R 0;
Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, vyakula na malisho. Kavu. Kilichofungwa vizuri. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
PHENOL ICSC: 0070
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE ISO RANGI HADI MANJANO AU PINKI ISIYOKOZA YENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Inapokanzwa, hutoa mafusho yenye sumu. Mmumunyo huu katika maji ni asidi dhaifu. Humenyuka pamoja na vioksidishaji kusababisha athari ya moto na mlipuko.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 5 ppm kama TWA; (ngozi); A4; BEI imetolewa; (ACGIH 2004).
MAK: kuingia kupitia kwa ngozi (H); Aina ya sarakani: 3B; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa haraka kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru waweza kufikiwa polepole kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii na mvuke huu husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi ya mvuke wake kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva, moyo na mafigo kusababisha degedege, kukosa fahamu, ugonjwa wa moyo kutoweza kupumua, kuzimia. Mfiduo huweza kuleta kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. Dutu hii huweza kuathiri ini na mafigo.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 182°C
Kiwango myeyuko: 43°C
Uzito wiani: 1.06 g/cm³
Umumunyifu katika maji: wastani
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 47
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.2
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.001
Kiwango cha kumweka: 79°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 715°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.36-10
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.46
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Nambari nyingine za UN: 2312 (iliyoyeuka); 2821 (inayomiminika). Matumizi ya vileo huongeza athari zinazodhuru. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya matibabu ya kuvuta hewa unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005