| |||||||||||||
| |||||||||||||
|
|||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Haiwaki lakini huongeza mwako wa dutu nyingine. Mimenyuko mingi yaweza kusababisha moto au kulipuka.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara. Usigusishe na maunzi yanayoweza kuwaka.
|
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
|
| MLIPUKO |
Hatari ya moto na mlipuko inapokanzwa au inapogusana na dutu za kuwaka (alkene, etha).
|
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka.
|
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
|
| MFIDUO |
|
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kuumwa kichwa. Kukosa pumzi. Kuumwa koo.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
|
Glavu za kuhami baridi.
|
UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Upofu.
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
|
|
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Endapo ni kimiminika: KAMWE usielekeze nyiri ya maji juu ya kioevu. (Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Ainisho ya EU Ainisho ya UN | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
|
Isodhurika kwa moto iwapo ndani ya jengo. Kinachotenganishwa na dutu zote. Baridi. Mara kwa mara ozoni huhifadhiwa kwenye jokofu ndani ya haloni.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: GESI ISO RANGI HADI BLUU YENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI KWA MWILI: Gesi hii ni nzito kuliko hewa. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapopata joto huzalisha oksijeni, ambayo huongeza athari ya moto. Dutu hii ni kioksidishaji madhubuti na humenyuka kwa ukali sana iwapo na maunzi yanayoweza kuwaka na yanayonakisi. Humenyuka na alkene, misombo ya kibenzini, kama vile anilini, na etha, bromini, misombo ya nitrojeni na mpira kuzalisha misombo isiyohimili mshtuko. Hushambulia metali isipokuwa dhahabu na platinam. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: (kazi kidogo) 0.1 ppm kama TWA; TLV: (moderate work) 0.08 ppm as TWA; TLV: (kazi nzito) 0.05 ppm kama TWA; A4; (ACGIH 2004). MAK: Aina ya sarakani: 3B; (DFG 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi yenye gesi hii kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Kuvuta pumzi yenye gesi hii kunaweza kusababisha pumu (tazama Vidokezo). Kioevu hiki huweza kusababisha jamidi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva, kusababisha kuumwa kichwa na upungufu wa umakini na utendaji. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Mapafu huathirika na mfiduo unaorudiwa au wa muda mrefu kwa gesi. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: -112°C Kiwango myeyuko: -193°C Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 0°C: 0.1 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 1.6 |
|||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa mimea.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya mnyunyuzio mwafaka unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. Aghalabu dalili za pumu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Kwa hiyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Mtu yeyote aliyeonyesha dalili za pumu kutokana na dutu hii kamwe asigusane na dutu hiyo tena. Pindua silinda ivujayo ili mvujio uwe juu kuzuia gesi isitoke katika hali ya uoevu.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||