NITROUS OXIDE ICSC: 0067
Mei 2003

Dinitrogen monoxide
Hyponitrous acid anhydride
Laughing gas
Dinitrogen oxide
(silinda)
CAS # 10024-97-2 N2O
RTECS # QX1350000 Masi ya molekuli: 44.0
UN # 1070 (iliyobanwa)
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki lakini huongeza mwako wa dutu nyingine. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO Hatari ya moto na mlipuko: Tazama Hatari za Kikemikali.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka.
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
MFIDUO
EPUKA MFIDUO KWA WANAWAKE (WAJAWAZITO)!

Kuvuta pumzi Kusikia raha (nishai). Kusinzia. Kupoteza fahamu.
Uingizaji hewa. Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
Glavu za kuhami baridi.
UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo. Mpeleke kwa matibabu.
Macho INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.

KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Ikiwa ni kioevu: usifyonze katika vumbi la mbao au vifyonzi vinginevyo viwakavyo. KAMWE usielekeze nyiri ya maji juu ya kioevu. Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 2.2
Jasara tanzu za UN: 5.1

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 20S1070
Isodhurika kwa moto iwapo ndani ya jengo. Kinachotenganishwa na maunzi yasiokubaliana. Tazama Hatari za Kikemikali. Baridi.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
NITROUS OXIDE ICSC: 0067
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
GESI OEVU ILIYOBANWA ISO RANGI YENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Gesi hii ni nzito kuliko hewa na huweza kujilimbikiza katika eneo ambalo dari liko chinichini na kusababisha upungufu wa oksijeni.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Humenyuka kwa ukali sana pamoja na anhidridi sulfurasi, amofasi boroni, fosfini, etha, alumini, hidrazini, fenili-lithiamu na kabaidi tangisteni kusababisha athari ya moto na mlipuko. Ikizi 300°C gesi hii ni kioksidishaji kikali na yaweza kutengeneza mchanganyiko ulipukao kukiwepo amonia, monoksidi kaboni, salfidi hidrojeni, mafuta, grisi na fueli.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 50 ppm kama TWA; A4; (ACGIH 2004).
MAK: 100 ppm, 180 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: II(2); Kundi la waja wazito lililo hatarini: D; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Kioevu hiki huweza kusababisha jamidi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva kusababisha kupungua kwa fahamu.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri uboho na mfumo wa neva wa pembeni. Inaweza kusababisha kusumisha kwa uzazi na kukua kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: -88.5°C
Kiwango myeyuko: -90.8°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.23 ifikapo -89°C
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 15°C: 0.15
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 5150
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 1.53
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.35
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Pindua silinda ivujayo ili mvujio uwe juu kuzuia gesi isitoke katika hali ya uoevu. Nambari nyingine ya UN: 2201 Kioevu baridi mno.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005