NITROBENZENE ICSC: 0065
Septemba 1993

Nitrobenzol
CAS # 98-95-3 C6H5NO2
RTECS # DA6475000 Masi ya molekuli: 123.1
UN # 1662
EC # 609-003-00-7
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizo wa maji, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 88°C. Hatari ya moto na mlipuko (tazama Hatari za Kikemikali).
Mfumo funge wa zaidi ya 88°C, uingizaji hewa.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Midomo au kucha kugeuka kuwa buluu. Ngozi kugeuka kuwa buluu. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kupoteza fahamu. Udhaifu.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho
Miwanivuli ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usifyonze katika vumbi la mbao au vifyonzi vinginevyo viwakavyo. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: T, N
R: 23/24/25-40-48/23/24-51/53-62
S: (1/2-)-28-36/37-45-61
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61S1662
Msimbo wa NFPA : H 3; F 2; R 0;
Kinachotenganishwa na dutu zenye kuungua na za kunakisi, vioksidishaji vikali, asidi kali, vyakula na malisho.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
NITROBENZENE ICSC: 0065
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU MANJANO ISIYOKOZA, KAMA MAFUTA CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Inapowaka hutengeneza mafusho yanayosababisha ulikaji, kama vile oksidi nitrojeni. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji vikali na vinakisishaji, kusababisha athari ya moto na mlipuko. Hushambulia aina fulani za plastiki. Hufanyiza kioksidishaji (kisichohimili moto) na misombo mingi ya kikaboni na iso-kikaboni, kama vile vioksidishaji, kloridi alumini na fenoli, anhidrasi ya hidroksidi potasiamu au na kiasi kidogo cha methanoli, anilini na glisero, pentakloridi fosforasi, asidi nitriki, asidi sulfuriki, potasiamu.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 1 ppm kama TWA; (ngozi); A3; BEI issued; (ACGIH 2004).
MAK: kuingia kupitia kwa ngozi (H); Aina ya sarakani: 3B; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kupitia kwenye ngozi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru waweza kufikiwa polepole kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C; wakati wa kutawanya, hata hivyo, kwa kazi zaidi.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii huweza kuathiri chembechembe za damu, kusababisha kufanyika kwa methemoglobin. Mfiduo husababisha kupungua fahamu. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri ogani zinazofanyiza damu. Yaweza kuwa na madhara kwa ini.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 211°C
Kiwango myeyuko: 6°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.2
Umumunyifu katika maji, g/100 ml: 0.2
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 20
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.2
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.00
Kiwango cha kumweka: 88°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 480°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.8-40
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.86
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Matumizi ya vileo huongeza athari zinazodhuru. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Usichukue nguo za kazi nyumbani. Wakati wa kuvukiza, USIVUKIZE yote hadi utupu uwepo chomboni kwa sababu kuna hatari ya kulipuka.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005