NICKEL CARBONYL ICSC: 0064
Oktoba 2001

Nickel tetracarbonyl
CAS # 13463-39-3 C4NiO4 / Ni(CO)4
RTECS # QR6300000 Masi ya molekuli: 170.7
UN # 1259
EC # 028-001-00-1
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua sana.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara. Usigusishe na vioksidishaji.
Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka. Hatari ya moto na mlipuko ikikanzwa zaidi ya 60°C. Kioevu na mvuke humweka kwenye mwanga.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. USITUMIE hewa iliyoshindiliwa kujaza, kutoa au kuchukua.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kuumwa kichwa. Kizunguzungu. Kichefuchefu. Kutapika. Kikohozi. Kukosa pumzi. Ngozi kugeuka kuwa bluu. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
Mfumo funge na uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Tazama Vidokezo.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Kisichoingiza hewa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi kikali cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: F, T+, N
R: 61-11-26-40-50/53
S: 53-45-60-61
Angalia: [E]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Jasara tanzu za UN: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: I
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Msimbo wa NFPA: H 4; F 3; R 3;
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GTF1-I
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, asidi kali, vyakula na malisho. Baridi. Weka gizani. Weka katika gesi ajizi.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
NICKEL CARBONYL ICSC: 0064
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI, VUKIVU, CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Huweza kulipuka wakati wa kukanza ifikapo 60°C. Dutu hii huweza kuwaka papo hapo inapogusana na hewa. Dutu hii hutengana inapogusana na asidi huzalisha monoksidi kaboni, gesi yenye sumu kali (ona ICSC 0023). Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji kusababisha athari ya moto na mlipuko. Inaoksidishwa na hewa kufanyiza zao ambalo huperoksidiwa huku kukiwa na hatari ya kusababisha moto.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV (kama Ni): 0.05 ppm; (kama TWA) (ACGIH 2001)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kupitia katika ngozi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva. Kuvuta pumzi ya mvuke wake kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Mfiduo huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Kuvuta hewa kwa kurudia au muda mrefu huweza kusababisha pumu. Dutu hii ina uwezekano wa kusababisha kansa kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 43°C
Kiwango myeyuko: -19°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.3
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 25.8°C: 53
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 5.9
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 3.0
Kiwango cha kumweka: <-20°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 60°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 2-34
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa viumbe hai vya majini.
VIDOKEZO
Hakujatokea jambo lolote kuhusu kulevya. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya matibabu ya kuvuta hewa unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. Aghalabu dalili za pumu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Kwa hiyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Mtu yeyote aliyeonyesha dalili za pumu kutokana na dutu hii kamwe asigusane na dutu hiyo tena. Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi. Suuza nguo zilizosibikwa (hatari ya moto) kwa maji mengi.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005