| |||||||||||||
| |||||||||||||
|
|||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
|
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
|
| MLIPUKO |
|
|
|
| MFIDUO |
|
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MGUSANO WOWOTE! EPUKA MFIDUO KWA WANAWAKE (WAJAWAZITO)!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kuumwa koo.
|
Uingizaji hewa (hapana kama ni poda), mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Wekundu.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
|
| Macho |
Wekundu.
|
Miwani ya usalama, kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Maumivu ya tumbo. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kutapika.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Vuta kiombwe maunzi yaliyomwagika. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru).
|
Ainisho ya EU Alama: Xn, N R: 22-40-42/43-50/53 S: (2-)-22-36/37-60-61 Ainisho ya UN | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
|
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: FUWELE MANJANO HADI KIJANI HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapokanzwa ifikapo 848°C huzalisha mafusho yenye sumu ya trioksidi sulfuri na monoksdi nikeli. Mmumunyo huu katika maji ni asidi dhaifu. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: kama Ni (kiwango cha kunuswa) 0.1 mg/m³ kama TWA; A4; (ACGIH 2004). MAK: (kiwango cha kunuswa); Sah; Aina ya sarakani: 1; (DFG 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Kuvuta hewa kwa kurudia au muda mrefu huweza kusababisha pumu. Mapafu huathirika na mfiduo unaorudiwa au wa muda mrefu kwa erosoli. Dutu hii huweza kuathiri kwa kusababisha uvimbe na kidonda kwa pua na nwazi wa fuvu. Dutu hii husababisha kansa kwa binadamu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango myeyuko (hutengana): 848°C Uzito wiani: 3.7 g/cm³ Umumunyifu katika maji: vizuri (29.3 g/100 ml ifikapo 0°C) |
|||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Aghalabu dalili za pumu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Kwa hiyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Mtu yeyote aliyeonyesha dalili za pumu kutokana na dutu hii kamwe asigusane na dutu hiyo tena. Usichukue nguo za kazi nyumbani. Mapendekezo kwenye kadi hii pia yanahusu Nickel sulfate hexahydrate (CAS 10101-97-0) na heptahydrate (CAS 10101-98-1).
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||