| |||||||||||||
| |||||||||||||
|
|||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Iwakayo endapo poda. Mafusho yenye sumu yaweza kufanyika kwenye moto.
|
|
Mchanga mkavu, USITUMIE dioksidi kaboni. USITUMIE maji.
|
| MLIPUKO |
Chembechembe zilizotawanyika hufanya mchanganyiko ulipukao hewani.
|
Zuia utuaji wa vumbi; mfumo funge, vifaa vya umeme na taa visivyolipuka kwa vumbi.
|
|
| MFIDUO |
|
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kukosa pumzi.
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko.
|
| Ngozi |
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
|
| Macho |
|
Miwani ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Vuta kiombwe maunzi yaliyomwagika. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru).
|
Ainisho ya EU Alama: Xn R: 40-43 S: (2-)-22-36 Ainisho ya UN | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
|
Kinachotenganishwa na asidi kali.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: MANGO METALI KAMA SILVA KATIKA MAUMBO MBALIMBALI HATARI KWA MWILI: Mlipuko wa vumbi huweza kutokea iwapo katika umbo la poda au punjepunje, vikichanganywa na hewa. HATARI ZA KIKEMIKALI: Humenyuka kwa nguvu ikiwa kwa poda na poda ya titaniamu na paklorati potasiamu, na vioksidishaji kama nitrati amoniamu kusababisha athari ya moto na mlipuko. Taratibu humenyuka pamoja na asidi isiyo ya kuoksidisha na kwa haraka pamoja na asidi vioksidishaji. Gesi na mvuke wa sumu yaweza kutoka kwa kuchomwa kwa nikeli (kama kabonili ya nikeli). VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: (kiwango cha kunuswa) 1.5 mg/m³ kama TWA; A5; (ACGIH 2004). MAK: (kiwango cha kunuswa); Sah; Aina ya sarakani: 1; (DFG 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi yenye vumbi. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Yaweza kusababisha muwasho wa mekaniko. Kuvuta pumzi yenye mafusho kunaweza kusababisha kichomi. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Kuvuta hewa kwa kurudia au muda mrefu huweza kusababisha pumu. Mapafu huathirika na mfiduo unaorudiwa au wa muda mrefu. Dutu hii ina uwezekano wa kusababisha kansa kwa binadamu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 2730°C Kiwango myeyuko: 1455°C Uzito wiani: 8.9 g/cm³ Umumunyifu katika maji: hakuna |
|||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kwa joto ya juu oksidi ya nikeli kwa mvuke yaweza kutoka. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Aghalabu dalili za pumu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Kwa hiyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Mtu yeyote aliyeonyesha dalili za pumu kutokana na dutu hii kamwe asigusane na dutu hiyo tena.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||