ETHYLENE GLYCOL MONOETHYL ETHER ICSC: 0060
Mei 2003

2-Ethoxyethanol
Monoethyl glycol ether
Oxitol
EGEE
Cellosolve
CAS # 110-80-5 C4H10O2 / CH3CH2OCH2CH2OH
RTECS # KK8050000 Masi ya molekuli: 90.1
UN # 1171
EC # 603-012-00-X
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizio wa maji, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 44°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 44°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
EPUKA MFIDUO KWA WANAWAKE (WAJAWAZITO)! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kikohozi. Kusinzia. Kuumwa kichwa. Kukosa pumzi. Kuumwa koo. Udhaifu. Kupoteza fahamu.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Kiwaa. Wekundu. Maumivu.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kichefuchefu. Kutapika. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Uingizaji hewa. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Osha salio kwa maji mengi. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni.
Kisichoingiza hewa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: T
R: 60-61-10-20/21/22
S: 53-45
Angalia: [E]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30GF1-III
Msimbo wa NFPA: H 2; F 2; R 0;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, vyakula na malisho. Weka gizani. Baridi.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ETHYLENE GLYCOL MONOETHYL ETHER ICSC: 0060
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI, KAMA MAFUTA CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii huweza kutengeneza peroksidi lipukaji. Humenyuka pamoja na vioksidishaji vikali kusababisha athari ya moto na mlipuko. Hushambulia aina fulani za plastiki na mpira.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 5 ppm (kama TWA); (ngozi); BEI taja kwa (ACGIH 2003).
MAK: 5 ppm, 19 mg/m³; H; Kundi la waja wazito lililo hatarini: B; Aina ya kiwango cha juu: II (8) (DFG 2002).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi kupitia kwenye ngozi, na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera kwa upole macho na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva, damu, uboho, mafigo na ini. Mfiduo wa viwango vya juu huweza kusababisha kupoteza fahamu. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Kioevu hukausha ngozi. Dutu hii huweza kuathiri damu na uboho kusababisha anemia na vidonda vya seli za damu. Inaweza kusababisha kusumisha kwa uzazi na kukua kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 135°C
Kiwango myeyuko: -70°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.93
Umumunyifu katika maji: kuchanganyika
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 0.5
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.1
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.00
Kiwango cha kumweka: 44°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 235°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: (at 93°C) 1.7-15.6
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -0.540
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi. Kagua kama kuna peroksidi kabla ya kunereka; iwapo chanya fanya iwe salama.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005