| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka katika hali mahususi. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
|
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
|
| MLIPUKO |
Hatari ya moto na mlipuko (tazama Hatari za Kikemikali).
|
Zuia mlimbiko wa chaji za umemetuamo (k.m. kwa kutuliza).
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kizunguzungu. Kusinzia. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Udhaifu. Kupoteza fahamu. Kifo.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Ngozi kavu. Wekundu. Mchomo.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
|
Miwanivuli ya usalama, kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Maumivu ya tumbo. (Tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Umpe maji mengi ya kunywa. Kupumzika.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni).
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Alama: Xn R: 40 S: (2-)-23-24/25-36/37 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: III | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61S1593 Msimbo wa NFPA : H 2; F 1; R 0; |
Kinachotenganishwa na metali (tazama Hatari za Kikemikali.), vyakula na malisho. Baridi. Uingizaji hewa kwenye sakafu.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI, CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI KWA MWILI: Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa. Kutokana na mtiririko, mchukucho n.k., chaji za kiumemetuamo huweza kutokea. HATARI ZA KIKEMIKALI: Inapogusana na nyuso zenye joto au mialimoto dutu hii hutengana na kutengeneza mafusho babuzi na yenye sumu. Humenyuka vikali ikiwa na metali kama vile poda za alumini na magnesiamu, besi kali na vioksidishaji vikali, kusababisha athari ya moto na mlipuko. Hushambulia aina fulani za plastiki, mpira na mipako. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 50 ppm kama TWA; A3; BEI imetolewa; (ACGIH 2004). MAK: Aina ya sarakani: 3A; (DFG 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Mfiduo husababisha kupungua fahamu. Mfiduo huweza kusababisha utengezwaji wa kaboksihimoglobini. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva and ini. Dutu hii ina uwezekano wa kusababisha kansa kwa binadamu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 40°C Kiwango myeyuko: -95.1°C Uzito wiani (maji = 1): 1.3 Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 1.3 Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 47.4 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.9 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.9 Jotoridi la kujiwasha: 556°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 12-25 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.25 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa maji ya ardhini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Ongezeko la kiasi kidogo cha dutu inayoweza kuwaka au kuzidi kwa kiasi cha oksijeni hewani kunazidisha uwakaji kwa nguvu. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi. Usitumie karibu na moto au uso moto, au wakati wa kulehemu. R30 ni jina la kibiashara.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||