METHANOL ICSC: 0057
Aprili 2000

Methyl alcohol
Carbinol
Wood alcohol
CAS # 67-56-1 CH4O / CH3OH
RTECS # PC1400000 Masi ya molekuli: 32.0
UN # 1230
EC # 603-001-00-X
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua sana. Tazama Vidokezo.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara. Usigusishe na vioksidishaji.
Poda, povu linalokinza alkoholi, maji mengi, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. USITUMIE hewa iliyoshindiliwa kujaza, kutoa au kuchukua. Tumia vifaa vya mkono visivyotoa cheche.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
EPUKA MFIDUO KWA VIJANA NA WATOTO!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Udhaifu. Kuona maruweruwe.
Uingizaji hewa. Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Ngozi kavu. Wekundu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kukosa pumzi. Kutapika. Degedege. Kupoteza fahamu. (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Osha salio kwa maji mengi. Ondoa mvuke kwa mnyunyuzio mwembamba wa maji. Vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: F, T
R: 11-23/24/25-39/23/24/25
S: (1/2-)-7-16-36/37-45
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Jasara tanzu za UN: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30S1230
Msimbo wa NFPA : H 1; F 3; R 0;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, vyakula na malisho. Baridi.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
METHANOL ICSC: 0057
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI, CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu huchanganyika vema na hewa, mchanganyiko unaolipuka hutokea kwa urahisi.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji kusababisha athari ya moto na mlipuko.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 200 ppm kama TWA, 250 ppm kama STEL; (ngozi); BEI imetolewa (ACGIH 2004).
MAK: 200 ppm, 270 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: II(4); kuingia kupitia kwa ngozi (H); Kundi la waja wazito lililo hatarini: C; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kupitia katika ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva, kusababisha upungufu wa fahamu. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva, kusababisha kuumwa kichwa cha kudumu au kinachorudiarudia na upungufu wa kuona.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 65°C
Kiwango myeyuko: -98°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.79
Umumunyifu katika maji: kuchanganyika
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 12.3
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 1.1
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.01
Kiwango cha kumweka: 12°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 464°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 5.5-44.
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -0.82/-0.66
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Huungua kutoa mwalimoto kibluu. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005