MERCURY ICSC: 0056
Aprili 2004

Quicksilver
Liquid silver
CAS # 7439-97-6 Hg
RTECS # OV4550000 Masi ya atomi: 200.6
UN # 2809
EC # 080-001-00-0
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO Hatari ya moto na mlipuko.

Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU! EPUKA MFIDUO KWA WANAWAKE (WAJAWAZITO)! EPUKA MFIDUO KWA VIJANA NA WATOTO!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Maumivu ya tumbo. Kikohozi. Kuhara. Kukosa pumzi. Kutapika. Homa au muinuko wa hali ya joto.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari endapo mwagiko ni mwingi. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo visivyo vya metali, vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
Maunzi maalum. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: T, N
R: 23-33-50/53
S: (1/2-)-7-45-60-61
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 8
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 80GC9-II+III
Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
MERCURY ICSC: 0056
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
METALI INAYOMIMINIKA, NZITO NA INA YA SILIVA, ISO HARUFU.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Inapokanzwa, hutoa mafusho yenye sumu. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na amonia na halojeni kusababisha athari ya moto na mlipuko. Hushambulia alumini na metali nyingine nyingi kutengeneza mchanganyiko mzito (amalgam).

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 0.025 mg/m³ kama TWA; (ngozi); A4; BEI imetolewa; (ACGIH 2004).
MAK: 0.1 mg/m³; kuhisisha ngozi (Sh); Aina ya kiwango cha juu: II(8); Aina ya sarakani: 3B; (DFG 2003).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake na kupitia kwenye ngozi, pia kama mvuke!

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera ngozi Kuvuta pumzi kwenye mvuke kunaweza kusababisha kubanwa kwa nguvu sana njia ya hewa na mapafu (pneumonitis). Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva na mafigo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva na mafigokusababisha kuwa na hasira, kukosa utulivu akilini, kutetemeka, mvurugiko wa akili, na kumbukumbu, tatizo la kuongea. Huweza kusababisha uvimbe na kubadilika rangi za fizi. Athari zinweza kuchelewa. Majaribio kwa wanyama yanaonyesha kuwa dutu hii huenda ikasababisha athari za sumu kwa uzazi na kukua kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 357°C
Kiwango myeyuko: -39°C
Uzito wiani (maji = 1): 13.5
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 0.26
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 6.93
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.009
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini. Kuzidisha kwa kemikali yaweza kutokea kwa samaki.
VIDOKEZO
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Hakuna onyo la harufu iwapo kuna vikolezi vya kitoksini. Usichukue nguo za kazi nyumbani.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005