LEAD ICSC: 0052
Oktoba 2002

Lead metal
Plumbum
(poda)
CAS # 7439-92-1 Pb
RTECS # OF7525000 Masi ya atomi: 207.2
UN #
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO Chembechembe zilizotawanyika hufanya mchanganyiko ulipukao hewani.
Zuia utuaji wa vumbi; mfumo funge, vifaa vya umeme na taa visivyolipuka kwa vumbi.

MFIDUO Ona ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA.
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MFIDUO KWA WANAWAKE (WAJAWAZITO)!

Kuvuta pumzi
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho
Miwani ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kichefuchefu. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P3 cha chembe zenye sumu).
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Kinachotenganishwa na vyakula na malisho na maunzi yasiokubaliana. Tazama Hatari za Kikemikali.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
LEAD ICSC: 0052
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
MANGO KIBLUU-NYEPE AU FEDHA KIJUVU KATIKA MAUMBO MBALIMBALI, HUGEUKA KUBADILIKA RANGI INAPOFIDULIWA NA HEWA.

HATARI KWA MWILI:
Mlipuko wa vumbi huweza kutokea iwapo katika umbo la poda au punjepunje, vikichanganywa na hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Inapokanzwa, hutoa mafusho yenye sumu. Humenyuka ikiwa na vioksidishaji. Humenyuka pamoja na asidi nitriki (moto na iliyokolea), asidi hidrokloriki iliyokolea na yanayochemka, na asidi sulfuriki. Ikishambuliwa kwa maji na asidi kikaboni dhaifu kuchanganyika pamoja na oksijeni.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 0.05 mg/m³ kama TWA; A3; BEI imetolewa; (ACGIH 2004).
MAK: Aina ya sarakani: 3B; Aina inayoleta mabadiliko kwa seli za uzazi: 3A; (DFG 2004).
EU OEL: kama TWA 0.15 mg/m³; (EU 2002).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Kikolezo cha chembechembe ya dhuru yaweza kufikiwa haraka ikitawanywa hasa kama poda.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri damu, uboho, mfumo mkuu wa neva, mfumo wa neva wa pembeni na mafigo, kusababisha anemia, adhari kwa ubongo (kama kifafa) (encephalopathy), ugonjwa wa neva wa pembeni, tumbo kuuma na kuharibika kwa figo. Husababisha kusumisha kwa uzazi na kukua kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 1740°C
Kiwango myeyuko: 327.5°C
Uzito wiani: 11.34 g/cm³
Umumunyifu katika maji: hakuna
DATA YA MAZINGIRA
Kuzidisha kwa kemikali yaweza kutokea kwa mimea na kwa mamalia. Inashauriwa sana kutoruhusu kemikali hii iingie kwenye mazingira.
VIDOKEZO
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Usichukue nguo za kazi nyumbani.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005