DICHLORODIFLUOROMETHANE ICSC: 0048
Machi 2002

Difluorodichloromethane
R 12
CFC 12
(silinda)
CAS # 75-71-8 CCl2F2
RTECS # PA8200000 Masi ya molekuli: 120.9
UN # 1028
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO

Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO


Kuvuta pumzi Mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida. Kuchanganyikiwa. Kusinzia. Kupoteza fahamu.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
Glavu za kuhami baridi.
UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.

KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Uingizaji hewa.
Silinda maalum isiyopitisha joto.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 2.2

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 20G2A
Kinachotenganishwa na maunzi yasiokubaliana. Tazama Hatari za Kikemikali. Baridi. Uingizaji hewa kwenye sakafu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
DICHLORODIFLUOROMETHANE ICSC: 0048
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
GESI OEVU ILIYOBANWA ISO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Gesi hii ni nzito kuliko hewa na huweza kujilimbikiza katika eneo ambalo dari liko chinichini na kusababisha upungufu wa oksijeni.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Inapogusana na nyuso zenye joto au mialimoto dutu hii hutengana na kutengeneza gesi babuzi na zenye sumu (kloridi hidrojeni ICSC 0163, fosjini ICSC 0007, floridi hidrojeni ICSC 0283, floridi kabonili ICSC 0633). Humenyuka kwa ukali sana pamoja na metali kama vile zinki na poda ya alumini. Hushambulia magnesiamu na aloi zake.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 1000 ppm kama TWA A4 (ACGIH 2001).
MAK: 1000 ppm; 5000 mg/m³; IV, C (DFG 2001).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Kisipodhibitiwa kioevu hiki huvukiza haraka sana na kusababisha ukifishwaji mno wa hewa na kuleta hatari kubwa ya kukosekana hewa katika maeneo funge.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Uvukizaji wa haraka wa kioevu huweza kusababisha jamidi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa moyo na mishipa na mfumo mkuu wa neva kusababisha ugonjwa wa moyo na kudidimia kwa mfumo mkuu wa neva. Mfiduo husababisha kupungua fahamu. Tazama Vidokezo.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: -30°C
Kiwango myeyuko: -158°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.5
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 0.03
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 568
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.2
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 2.16
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa mgongano kwa kanda ya ozoni.
VIDOKEZO
Ukolezi mkubwa katika hewa husababisha unakisi wa oksijeni pamoja na hatari ya kupoteza fahamu au kufa. Pima kiasi cha oksijeni kabla ya kuingia katika eneo. Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi. Usitumie karibu na moto au uso moto, au wakati wa kulehemu. Pindua silinda ivujayo ili mvujio uwe juu kuzuia gesi isitoke katika hali ya uoevu. Freon 12, Frigen 12, Halon 12 ni majina ya kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005