ETHYLENE DIBROMIDE ICSC: 0045
Aprili 1993

1,2-Dibromoethane
EDB
CAS # 106-93-4 Br(CH2)2Br / C2H4Br2
RTECS # KH9275000 Masi ya molekuli: 187.9
UN # 1605
EC # 602-010-00-6
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO Hatari ya moto na mlipuko inapogusana na poda ya metali: tazama Hatari za Kikemikali.


MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Mchomo. Kikohozi. Kupumua kwa shida. Kukosa pumzi. Kupoteza fahamu.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. Maumivu. Malengelenge.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Msokoto wa tumbo. Kuchanganyikiwa. Kuhara. Kuumwa kichwa.


KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga kavu au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: T, N
R: 45-23/24/25-36/37/38-51/53
S: 53-45-61
Angalia: [E]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61S1605
Msimbo wa NFPA : H 3; F 0; R 0;
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, besi kali, poda ya metali, vyakula na malisho: tazama Hatari za Kikemikali. Kavu. Weka gizani. Uingizaji hewa kwenye sakafu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ETHYLENE DIBROMIDE ICSC: 0045
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Inapogusana na nyuso zenye joto au miali ya moto dutu hii hutengana na kutengeneza mafusho babuzi na yenye sumu, bromidi hidrojeni (tazama ICSC 0282) na bromini (tazama ICSC 0107). Dutu hii hutengana polepole inapoathiriwa na mwanga au unyevu huzalisha bromidi hidrojeni yenye babuzi. Humenyuka kwa nguvu pamoja na poda ya alumini au magnesiamu, metali kama vile sodiamu, potasiamu na kalsiamu, besi kali na vioksidishaji vikali, kusababisha athari ya moto na mlipuko. Hushambulia shahamu, mpira, baadhi ya plastiki na mipako.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: (skin); A3; (ACGIH 2004).
MAK: kuingia kupitia kwa ngozi (H); Aina ya sarakani: 2; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva, kusababisha kupungua kwa fahamu.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mapafu huathirika na mfiduo unaorudiwa au wa muda mrefu kusababisha ugonjwa wa mapafu. Dutu hii huweza kuathiri ini na mafigo. Dutu hii huenda inasababisha kansa kwa binadamu. Majaribio kwa wanyama yanaonyesha kuwa dutu hii huenda ikasababisha athari za sumu kwa uzazi wa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 131°C
Kiwango myeyuko: 10°C
Uzito wiani (maji = 1): 2.2
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: mbaya
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 1.5
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 6.5
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.08
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.93
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa maji.
VIDOKEZO
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005