ETHANOL (ANHYDROUS) ICSC: 0044
Oktoba 2000

Ethyl alcohol
CAS # 64-17-5 CH3CH2OH / C2H6O
RTECS # KQ6300000 Masi ya molekuli: 46.1
UN # 1170
EC # 603-002-00-5
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua sana.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara. Usigusishe na vioksidishaji vikali.
Poda, povu linalokinza alkoholi, maji mengi, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. USITUMIE hewa iliyoshindiliwa kujaza, kutoa au kuchukua.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO


Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa kichwa. Uchovu. Kusinzia.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi Ngozi kavu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu. Maumivu. Kuungua.
Miwanivuli ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Mchomo. Kuumwa kichwa. Kuchanganyikiwa. Kizunguzungu. Kupoteza fahamu.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Uingizaji hewa. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Osha salio kwa maji mengi.
Ainisho ya EU
Alama: F
R: 11
S: (2-)-7-16
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30S1170
Msimbo wa NFPA : H 0; F 3; R 0;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ETHANOL (ANHYDROUS) ICSC: 0044
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI, CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu huchanganyika vema na hewa, mchanganyiko unaolipuka hutokea kwa urahisi.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Humenyuka pole pole pamoja na hipokloriti kalsiamu, oksidi silva na amonia kusababisha athari ya moto na mlipuko. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji vikali kama vile asidi nitriki, nitrati silva, nitrati zebaki au pakloreti magnesiamu kusababisha athari ya moto na mlipuko.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 1000 ppm kama TWA; A4; (ACGIH 2004).
MAK: 500 ppm, 960 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: II(2); Aina ya sarakani: 5; Aina inayoleta mabadiliko kwa seli za uzazi: 5; Kundi la waja wazito lililo hatarini: C; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru waweza kufikiwa polepole kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho. Kuvuta pumzi ya mvuke wake wa kiwango cha juu kunaweza kusababisha muwasho machoni na kwenye mfumo wa upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Kioevu hukausha ngozi. Dutu hii huweza kuathiri sehemu za awali za njia ya upumuaji na mfumo mkuu wa neva, kusababisha ukereketwaji, kuumwa kichua, uchovu na upungufu wa utulivu. Tazama Vidokezo.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 79°C
Kiwango myeyuko: -117°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.8
Umumunyifu katika maji: kuchanganyika
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 5.8
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 1.6
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.03
Kiwango cha kumweka: 13°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 363°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 3.3-19
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -0.32
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Unywaji wa ethanoli wakati wa mimba waweza kuathiri vibaya mtoto aliye tumboni. Unywaji wa ethanoli wa muda mrefu waweza kusababisha ini kuwa gumu. Kiwango cha kumweka ni 24°C ikiwa mmumunyo na maji 50%.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005