| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 31°C.
|
Mfumo funge wa zaidi ya 31°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Mchomo. Kikohozi. Kuumwa koo. Kuumwa kichwa. Kupumua kwa shida. Kichefuchefu. Kukosa pumzi. Kutapika. Tetemeko. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. Mibabuko nzito ya ngozi. Mchomo. Maumivu. Malengelenge.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Maumivu. Wekundu. Upofu wa kudumu. Kuungua kunakopenya sana.
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Msokoto wa tumbo. Mchomo kooni na kifuani. Kuhara. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kuumwa koo. Kutapika. Mshtuko au kuzimia.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Umpe maji mengi ya kunywa. Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
|
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Alama: T R: 45-10-23/24/25-34-43 S: 53-45 Angalia: [E] Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Jasara tanzu za UN: 3 Kikundi Ufungashaji cha UN: II | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61S2023 Msimbo wa NFPA: H 3; F 3; R 2; |
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, asidi, besi, alumini, zinki, amini, vyakula na malisho. Kilichofungwa vizuri.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hupolimisha kutokana na kukanza au kwa kuathiriwa na asidi kali, besi kali. Inapowaka hutengeneza mafusho babuzi na yenye sumu, kloridi hidrojeni (tazama ICSC0163) na mafusho ya klorini (tazama ICSC0126). Humenyuka kwa ukali sana ikiwa na vioksidishaji vikali. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na alumini, zinki, alkoholi, fenoli, amini (hasa anilini), na asidi kikaboni kusababisha athari ya moto na mlipuko. Hushambulia chuma kukiwepo maji. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 0.5 ppm kama TWA; (ngozi); A3; (ACGIH 2003). MAK: H; Sh; Aina ya sarakani: 2; Aina inayoleta mabadiliko kwa seli za uzazi: 3B; (DFG 2003). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho ngozi na njia ya upumuaji. Husababisha ubabuzi inapomezwa. Kuvuta pumzi yenye mvuke kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Kuvuta pumzi yenye mvuke kunaweza kusababisha pumu (tazama Vidokezo). Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva, mafigo na ini kusababisha degedege, kuharibika kwa figo, kuharibika kwa ini. Mfiduo wa viwango vya juu huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Dutu hii huweza kuathiri mafigo, ini na mapafu kusababisha kuharibika kwa utendaji. Dutu hii huenda inasababisha kansa kwa binadamu. Majaribio kwa wanyama yanaonyesha kuwa dutu hii huenda ikasababisha athari za sumu kwa uzazi na kukua kwa binadamu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 116°C Kiwango myeyuko: (tazama Vidokezo) -48°C Uzito wiani (maji = 1): 1.2 Umumunyifu katika maji, g/100 ml: 6 Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 1.6 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.2 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.05 Kiwango cha kumweka: 31°C c.c. Jotoridi la kujiwasha: 385°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 3.8-21 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.26 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Viwango myeyuko vinginevyo: -25.6 °C na -57°C. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya matibabu ya kuvuta hewa unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi. Usichukue nguo za kazi nyumbani.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||