| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua sana.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara. Usigusishe na vioksidishaji vikali. Usigusishe na nyuso za moto.
|
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizo wa maji, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka. Hatari ya moto na mlipuko inapogusana na maunzi yasiokubaliana: tazama Hatari za Kikemikali.
|
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. Zuia mlimbiko wa chaji ya mtuamo umeme (k.m. kwa kutuliza). USITUMIE hewa iliyoshindiliwa kujaza, kutoa au kuchukua. Tumia vifaa vya mkono visivyotoa cheche.
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Maumivu ya tumbo. Kikohozi. Kizunguzungu. Kuzinzia. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kuumwa koo. Kupoteza fahamu. Kutapika.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Watery eyes.
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
(zaidi tazama Uvutaji pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Osha salio kwa maji mengi. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Kisichoingiza hewa. Ainisho ya EU Alama: F, Xn R: 11-19-36/37-40-66 S: (2-)-9-16-36/37-46 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 3 Kikundi Ufungashaji cha UN: II | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30S1165 Msimbo wa NFPA : H 2; F 3; R 1; |
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, asidi kali. Baridi. Kavu. Weka gizani. Hifadhi iwapo tu imetulia.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI , CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI KWA MWILI: Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana. Kutokana na mtiririko, mchukucho n.k., chaji za kiumemetuamo huweza kutokea. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii huweza kutengeneza peroksidi lipukaji. Humenyuka kwa nguvu ikiwa na vioksidishaji vikali na asidi kali iliokelea. Humenyuka kwa mlipuko pamoja na baadhi ya vichocheo, (kama vile Raney-nikeli zaidi ya 210°C). Hushambulia plastiki nyingi. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 20 ppm kama TWA; (ngozi); A3; (ACGIH 2004). MAK: 20 ppm, 73 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: I(2); kuingia kupitia kwa ngozi (H); Aina ya sarakani: 4; Kundi la waja wazito lililo hatarini: D; (DFG 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake na kupitia kwenye ngozi. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C; wakati wa kunyunyiza kwa kasi zaidi. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva, ini na mafigo. Mfiduo ukolezi mkubwa ya mvuke huweza kusababisha kupoteza fahamu. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Kioevu hukausha ngozi. Dutu hii huenda inasababisha kansa kwa binadamu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 101°C Kiwango myeyuko: 12°C Uzito wiani (maji = 1): 1.03 Umumunyifu katika maji: kuchanganyika Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 4.1 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.0 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.08 Kiwango cha kumweka: 12°C Jotoridi la kujiwasha: 180°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 2-22.5 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -0.42 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Matumizi ya vileo huongeza athari zinazodhuru. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi. Kagua kama kuna peroksidi kabla ya kunereka; iwapo chanya fanya iwe salama.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||