| |||||||||||||
| |||||||||||||
|
|||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka.
|
Usiwashe moto.
|
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizio wa maji, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 93°C.
|
Mfumo funge wa zaidi ya 93°C, uingizaji hewa.
|
|
| MFIDUO |
|
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU! EPUKA MFIDUO KWA WANAWAKE (WAJAWAZITO)!
|
|
| Kuvuta pumzi |
|
Uingizaji hewa.
|
Hewa safi, mapumziko.
|
| Ngozi |
Ngozi kavu.
|
Glavu za kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
|
| Macho |
|
Miwani ya usalama.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Osha salio kwa maji mengi.
|
Ainisho ya EU Alama: Xn R: 63 S: (2-)-36/37 Ainisho ya UN | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Msimbo wa NFPA: H 1; F 2; R 0;
|
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali. Uingizaji hewa kwenye sakafu.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii huenda ikatengeneza peroksidi lipukaji. Humenyuka pamoja na vioksidishaji vikali. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV haifahamiki. MAK haijathibitishwa. |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Kioevu hukausha ngozi. Majaribio kwa wanyama yanaonyesha kuwa dutu hii huenda ikasababisha athari za sumu kwa uzazi na kukua kwa binadamu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 193°C Uzito wiani (maji = 1): 1.04 Umumunyifu katika maji: vizuri sana Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 30 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.1 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.001 Kiwango cha kumweka: 93°C o.c. Jotoridi la kujiwasha: 215°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.6-18.1 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -1.14/-0.93 (imekadiriwa) | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Methyl carbitol, Poly-Solv DM, Methyl Digol na Dowanol DM ni majina ya kibiashara. Kagua kama kuna peroksidi kabla ya kunereka; iwapo chanya fanya iwe salama.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||