DIBUTYL PHTHALATE ICSC: 0036
Machi 2002

1,2-Benzenedicarboxylic acid dibutyl ester
Di-n-butyl phthalate
CAS # 84-74-2 C16H22O4 / C6H4(COOC4H9)2
RTECS # TI0875000 Masi ya molekuli: 278.3
UN # 3082
EC # 607-318-00-4
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka.
Usiwashe moto.
Povu, poda kavu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU! EPUKA MFIDUO KWA WANAWAKE (WAJAWAZITO)!

Kuvuta pumzi
Uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kuhara. Kichefuchefu. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vyenye mifuniko. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchangavermiculite au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
Ainisho ya EU
Alama: T, N
R: 61-62-50
S: 53-45-61
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 9
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Msimbo wa NFPA: H 0; F 1; R 0;
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 90GM6-III
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
DIBUTYL PHTHALATE ICSC: 0036
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KINATACHO KISICHO RANGI HADI MANJANO CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Kutokana na mtiririko, mchukucho n.k., chaji za kiumemetuamo huweza kutokea.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha mafusho yawashayo na yenye sumus (anhidridi ya ftaliki, ICSC 0315). Humenyuka ikiwa na vioksidishaji vikali.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 5 mg/m³ kama TWA (ACGIH 2001).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru hautafikiwa au utafikiwa polepole sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Majaribio kwa wanyama yanaonyesha kuwa dutu hii huenda ikasababisha athari za sumu kwa uzazi na kukua kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 340°C
Kiwango myeyuko: -35°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.05
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 25°C: 0.001
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: < 0.01
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 9.58
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.00
Kiwango cha kumweka: 157°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 402°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 0.5 (ifikapo 235°C) hadi 2.5
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 4.72
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO

MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005