1-DECANETHIOL ICSC: 0035
Aprili 2004

Decyl mercaptan
CAS # 143-10-2 C10H21SH
RTECS # Masi ya molekuli: 174.3
UN #
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Povu, dioksidi kaboni, poda.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 98°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 98°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.

MFIDUO


Kuvuta pumzi Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Kuungua kunakopenya sana. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Kichefuchefu. Kutapika. Kizunguzungu. Kusinzia. Kuumwa kichwa. Udhaifu.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Msimbo wa NFPA: H 2; F 2; R 0;
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, besi kali.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
1-DECANETHIOL ICSC: 0035
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha gesi zenye sumu pamoja na dioksidi sulfuri (tazama ICSC 0074). Humenyuka pamoja na besi kali na vioksidishaji vikali.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
MAK haijathibitishwa.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 241°C
Kiwango myeyuko: -26°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.84
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: <10
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 6.0
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.00
Kiwango cha kumweka: 98°C
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO

MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005