DDT ICSC: 0034
Aprili 2004

Dichlorodiphenyltrichloroethane
1,1,1-Trichloro-2,2-bis(p-chlorophenyl)ethane
2,2-bis(p-Chlorophenyl)-1,1,1-trichloroethane
1,1'-(2,2,2-Trichloroethylidene)bis(4-chlorobenzene)
p,p'-DDT
CAS # 50-29-3 C14H9Cl5
RTECS # KJ3325000 Masi ya molekuli: 354.5
UN # 2761
EC # 602-045-00-7
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Michanganyiko ya vioevu vyenye vimumunyisho vya kaboni huweza kuwaka (moto). Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU! EPUKA MFIDUO KWA WANAWAKE (WAJAWAZITO)!

Kuvuta pumzi Kikohozi.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Kutetemeka. Kuhara. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kutapika. Kufa ganzi. Kuchangamka mno. Paresthesias. Degedege.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vinavyokalafatika visivyo vya metali; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P3 cha chembe zenye sumu.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi kikali cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: T, N
R: 25-40-48/25-50/53
S: (1/2-)-22-36/37-45-60-61
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GT7-III
Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Kinachotenganishwa na chuma, alumini na chumvi zake, vyakula na malisho. Tazama Hatari za Kikemikali.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
DDT ICSC: 0034
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE ZISIO NA RANGI AU PODA NYEUPE. BIDHAA YA KIUFUNDI NI NTA NGUMU.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Inapowaka hutengeneza mafusho babuzi na yenye sumu kama vile kloridi hidrojeni. Humenyuka pamoja na alumini na chuma.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 1 mg/m³; kama TWA; A3 (imethibitishwa kuwa kasinojeni kwa wanyama na haijulikana kama ina athari kwa wanadamu); (ACGIH 2004).
MAK: 1 mg/m³; kuingia kupitia kwa ngozi (H); Aina ya kiwango cha juu: II(8); (DFG 2003).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka hasa iwapo katika hali ya poda.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Yaweza kusababisha muwasho wa mekaniko. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva kusababisha degedege na matatizo ya kupumua. Mfiduo wa viwango vya juu huweza kusababisha kifo. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva na ini. Dutu hii ina uwezekano wa kusababisha kansa kwa binadamu. Majaribio kwa wanyama yanaonyesha kuwa dutu hii huenda ikasababisha athari za sumu kwa uzazi na kukua kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 260°C
Kiwango myeyuko: 109°C
Uzito wiani: 1.6 g/cm³
Umumunyifu katika maji: mbaya
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 6.36
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa ndege. Kuzidisha kwa kemikali yaweza kutokea kwa mfano kufuata mwishono wa vyakula kwa maziwa na viumbe viishivyo majini. Dutu hii huingia katika mazingira kwa matumizi ya kawaida. Utaratibu wa hali ya juu lazima unahitajika ili kuzuia kiasi zaidi kisitokee kama kupitia kwa kutupwa ovyo.
VIDOKEZO
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Vimumunyishaji chukuzi vitumikavyo katika misombo ya kibiashara vyaweza kubadilisha tabia za kimaumbile na za kitoksini. Usichukue nguo za kazi nyumbani. Shauri sheria za nchi. Agritan, Azotox, Anofex, Ixodex, Gesapon, Gesarex, Gesarol, Guesapon, Clofenotane, Zeidane, Dicophane, Neocid ni majina ya kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005